DAR ES SALAAM. Taarifa iliyotolewa leo Februari 10, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema kuwa Rais amempandisha cheo Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza leo.
Kabla ya uteuzi huu Kamishna Haji alikuwa mhasibu mkuu wa Polisi Zanzibar.
Kamishna huyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.
Hivi karibuni kumekuwepo na mjadara wa kimamlaka kuhusiana na mamlaka aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upade wa bara na Zanzibar ambapo Waziri wa katiba na sheria aliweka wazi na kusema Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni John Pombe Magufuri anayo mamlaka ya kuteua na upande wowote wa Jamhuri.
Post a Comment