UTAFITI.
Uchunguzi wa kina wa sayansi
unaonyesha kuwa Muingereza wa kwanza kutoka miaka 10,000 iliyopita alikuwa na
ngozi nyeusi na macho ya rangi ya samawati,
watafiti kutoka jumba la ukumbusho wa
historia asilia mjini London wamepata chembechembe za vina saba vya Cheddar
Man, mifupa ya zamani zaidi ya Muingereza iliyogunduliwa mnamo mwaka 1903.
PHOTO: Surah ii imeundwa kwa mfumo wa picha za 3D za mifupa na
taarifa kuhusu chembe chembe za DNA za mwanamme huyo.
|
Watafiti
hao kutoka chuo kikuu cha University College London baadaye walitumia uchambuzi
wa vina saba kusaidia kuunda upya sura yake, ambapo ilidhihirisha kwamba ngozi
nyeupe miongoni mwa Wazungu wa sasa ni jambo la miaka ya hivi karibuni.
Imefahamika
kuwa hakuna Muingireza kabla ya historia hii aliyewahi kuchambuliwa kwa namna
hii, hivyo kutokana na hili uchambuzi huu unatoa mwanga muhimu kuhusu watu wa
kwanza walioishi Uingereza.
Mifupa
ya Cheddar Man ilifukuliwa miaka 115 iliyopita katika pango la Gough, lililoko
huko Cheddar Gorge. Utafiti uliofuata ulidhihirisha kwamba alikuwa na kimo
kifupi akilinganishwa na viwango vya leo - kiasi cha ft5 in5 - na huenda
alifariki akiwa na takriban miaka 20.
PHOTO: Prof. Chris Stringer ambaye alimfanyia utafiti Cheddar Man
kwa takribani miaka 40 alishangazwa na uundaji mpya wa sura ya Cheddar Man.
|
Profesa Chris Stringer, mtafiti kiongozi wa jumba hilo la ukumbusho kuhusu asili ya binadamu amesema: "nimekuwa nikifanya uchunguzi wa mifupa ya Cheddar Man kwa miaka 40, kwa hiyo kuona sasa sura kama inavyoonekana kwa jamaa huyu, nywele, uso, rangi ya macho na mwili, ni jambo ambalo hatungelifikiria miaka michache iliyopita, na licha ya hayo hilo ndilo linaloonyeshwa na data za sayansi."
Kwenye kicha cha Cheddar Man kuna nyufa kwenye fuvu la kichwa zinazoashilia huenda alifariki
katika mazingira ya ghasia, haijulikani ni vipi alivyoishia ndano ya pango
hilo, lakini inawezekana aliwekwa hapo na wenzake katika jamii anayotoka.
Waligundua
kuwa muingreza huyo alikuwa na nywele nyeusi - na uwezekano mdogo kwamba
zilikuwa za ondo -macho ya rangi ya samawati na ngozi iliyo nyeusi. Sio jambo
la kustaajabisha kwamba utafiti huu umewavutia wengi katika mitandao ya
kijamii.
PHOTO: Mifupa ya Cheddar Man kwa sasa imewekwa kwenye pango la
Gough nchini humo.
|
Utafiti huu umefichua kuwa Cheddar Man alikuwa na uhusiano na waliokuwa anajulikana kama wawindaji na wakusanyaji wa Maghribi - waliofanyiwa uchunguzi Uhispania Luxembourg na Hungary.
Wasanii
wa uholanzi Alfons na Adrie Kennis, walitumia matokeo ya jini na kuyaunganisha
na vipimo vya mwili kutokana na picha za fuvu la kichwa. Matokeo yake yalikuwa
ni muundo wa sura ya kizazi cha nyuma.
Huenda
ngozi nyeupe ilianza kuonekana Uingereza kwa uhamiji kutoka mashariki ya kati
miaka 6000 iliyopita. Idadi ya watu hawa waikuwa na ngozi nyeupe na macho ya
rangi ya kahawia na kuingiliana na jamii kama anayotoka Cheddar Man.
"Huenda kuna vigezo vingine
vinavyosababisha kupungua kwa rangi ya ngozi katika muda wa miaka 10,000 iliyopita,
lakini huo ndio ufafanuzi wanaotumia baadhi ya wanasayansi," amesema Prof Thomas.
Matokeo
ya utafiti huo pia yameonyesha kuwa Cheddar Man hakuweza kunywa maziwa akiwa mtu mzima.
Uwezo huu ulisambaa baadaye katika kizazi kilichofuata. Asilimia
10 ya kizazi cha wazungu wa sasa kinatokana na jamii kama ya Cheddar Man.
source: BBC
Post a Comment