Dar Es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Februari, 2018 saa 3:00 asubuhi atawaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa watakaoapishwa ni Mhe. Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana tarehe 15 Februari, 2018.
PHOTO: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (kushoto) I akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (kushoto) akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiashuhudia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kula kiapo kuwa mabalozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Post a Comment