0



HARARE.


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani saa chache baada ya jeshi la Zimbabwe kutwaa madaraka, kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari nchini Afrika Kusini.
"Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani," mtandao wa habari wa News24 uliandika bila ya kutoa taarifahkwa undani. 
Misukusuko ya kisiasa imekuwa ikiongezeka tangu Rais Mugabe hivi majuzi alipomfuta na kumuondoa oazini bwana Emmerson Mnangagwa pichani juu, ambaye alikuwa mshirika wake wa miaka mingi kama makamu wa Rais.

Ubalozi wa Marekani:  Umewataka wananchi wa Marekani wanaoishi nchini humo kubaki majumbani mwao pasi kutoka.
Katika taarifa yake, balozi wa Marekani mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, amewataka wananchi wa Marekani wanaoishi nchini Zimbabwe kusalia makwao. Pia alirusha ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akisema "Kutokana na hali tete nchini Zimbabwe, wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani mjini Harare watapunguzwa na kufungwa kwa umma Novemba 15. Wafanyakazi wa Ubalozi wataendelea kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Zimbabwe. "
Ubalozi wa Uingereza: umewataka raia wa nchi hiyo waishio Zimbabwe kusalia makwao.
Ubalozi wa Canada: umetangaza kufungwa kwa ofisi zake baada ya hotuba ya kijeshi.

Post a Comment

 
Top