DAR ES SALAAM.
Na. Christina Mwagala.
Mkutano wa 33 wa jumuiya ya tawala za
mikoa nchini (ALAT) uliokuwa ufanyike jijini Mbeya na baadaye kuhamishiwa
jijini Dar Es Salaam umeanza leo kwa baadhi ya wanchama wa mkutano huo kufanya
maandalizi yatokanayo na ajenda muhimu zitakazojadiliwa mapema kesho mara baada
ya ufunguzi.
![]() |
PHOTO: Mstahiki meya wa jiji la Dar Es Salaam
Isaya Mwita (kushoto) akiongea wakati wa
mkutano mkuu wa ALAT jijini Dar Es Salaam. |
Mwenyeji wa mkutano wa 33 wa Jumuiya ya
Tawala na Serikali za Mitaa ALAT ambaye ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita amesema kupitia mkutano huo wataiomba serikali ili iweze
kurudisha vyanzo vya mapato vilivyokuwa katika halmashauri.
Meya Mwita alizungumza kauli hiyo wakati
akitoa salamu za kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa ALAT unaofanyika jijini
Dar Es Salaam badala ya Mkoani Meya, alisema vyanzo vya mapato ambavyo vilikuwa
vikisimamiwa na halmashauri, majiji viliwezesha kuleta maendeleo katika nyanja
mbalimbali hususani huduma za kijamii.
Alifafanua kuwa vyanzo hivyo kuwa ni
matangazo ya barabarani sambamba na kodi za majego ambapo kwa kiasi kikubwa
zilikuwa zikiiletea halmashauri fedha ambazo zilitumika kuboresha huduma za
afya, elimu na barabara.
Aliongeza kuwa kwakuzingatia ustawi wa
halmashauri hizo ,mkutano huo utajadili na kumfikishia Rais Dk. John Magufuli
ili fedha hizo zirudi kwa ajili ya maendeleo hususani Vijijini, Kata na Majiji.
![]() |
| PHOTO: Baadhi ya wanachama, Wakurugenzi, Meya na Maofisa wa wilaya nchini. |
“Hali
ya Halmashauri nyingi kifedha sio nzuri, na hii ni baada ya vyanzo hivi vya
mapato ambavyo tulikuwa tunategemea kuchukuliwa, katika hali yoyote hakuna
halmashauri ambayo itakuwa na fedha” alisema Meya
Mwita.
Akitolea mfano halmashauri ya Ilala
iliyopo jijini Dar es Salaam kuwa kupitia vyanzo hivyo ilikuwa ikikusanya zaidi
ya bilioni 68 ambazo zilikuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma za kijamii
ndani ya halmashauri hiyo.
Aitha alisema kuwa mbali na changamoto za
mapato ambazo halimashauri zinakabiliana nazo,alizungumzia changamoto nyingine
ni kuhusu hali za madiwani hususani kwenye fedha kuwa imekuwa ngumu.
Alisema “hali ya madiwani kifedha
imekuwa ngumu katika utendaji wao wa kila siku kwasababu wanalipwa shilingi
350,000, ambazo hazitoshi, kutokana na gharama za usafiri anazotumia kuzungukia
maeneo yake”


Post a Comment