0
DAR ES SALAAM. 
KWA UFUPI.
...
...
Mahafali ya nane ya bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini  PSPTB yamefanyika jijini Dar Es Salaam ambapo zaidi ya wahitimu 303 wa cheti cha awali, cheti cha msingi pamoja na cheti cha ununuzi na ugavi waliweza kuhitimu  na kupata nafasi ya kukabidhiwa vyeti vyao ikiwa ni pamoja na kula kiapo cha utumishi mwema pale watakapokuwa kazini.

PHOTO: Viongozi na mgeni rasmi wakiwaongoza wahitimu katika gwaride kuelekea katika eneo maalumu la mahafali yao ya nane yaliyofanyika katika viwanja vya karimjee jijini Dar Es Salaam.

PHOTO: Mgeni rasmi Amina Shaban akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza sherehe za mahafali. 

PHOTO: Wahitimu wakipewa maelekezo jinsi ya kula kiapo cha utendaji unaofuata sheria katika shuguli za ununuzi na ugavi pasi kupokea rushwa. 


PHOTO: Amina Khamis Shaaban (aliyemwakilisha Dkt Ashatu Kijaji) akiongea na wahitimu wakati wa mahafali hayo. 

PHOTO: Wahitimu wakivaa kofia zao ikiwa ni kipengere cha kuhitimu na kutunukiwa cheti.

PHOTO: (kulia) Ismail mwita ambaye ni mjumbe wa bodi wa PSPTB akiwa ni mmoja wawaliopewa cheti kutokana na mgeni rasmi (wa tatu kutoka kulia) 



PHOTO: Wahitimu wa nafasi ya cheti wapatao 280 wakiwa wamesemama mara baada ya kutunukiwa. 


PHOTO: Wahitimu wa nafasi ya cheti cha msingi wapatao 23 ambao kwa pamoja wamesimama baada ya kutunukiwa. 

PHOTO: Blassband iliyokuwepo kufanikisha kuongoza na utolewaji wa vyeti pamoja na kuimba nyimbo tofauti katika sherehe hiyo. 


PHOTO: Ndugu na jamaa wa wahitimu waliofika kuwasindikiza ndugu zao waliohitimu elimu ya ununuzi na ugavi. 


PHOTO: Moja ya picha ya pamoja ya wahitimu waliyopiga na viongozi wa bodi,  mgeni rasmi kwa ajili ya kumbukumbu.

Picha: Leonard Mutani.



HABARI KWA UNDANI HII HAPA CHINI
...
...
Akifungua sherehe za mahafali hayo, mwenyekiti wa bodi ya ununuzi na ugavi Sr. Dkt. Hellen Bandiho amesema kuwa bodi inaendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini ambapo kati ya watahiniwa 3086 waliofanya mitihani, 1,101 wamefaulu.

"kutokana na mtaala wa bodi kutambulika na kuthibitishwa na taasisi ya kimataifa ya IFPSM, wahitimubwa leo wa ngazi ya CPSP watatunukiwa vyeti viwili,  yaani cheti chetu cha CPSP na cha IFPSM. Hii ni hatua kubwa katika kuwatambulisha wahitimu wetu katika soko ajira kimataifa". Alisema Sr. Dkt. Hellen Bandiho

Pia ametanabaisha kuwa wakati bodi hiyo uwapa miongozo ya maadili ya kitaaluma kwa kushirikiana na vyuo vya mafunzo ya juu yameimizwa kuanzishwa kwa mafunzo mapya hali inayopelekea bodi hiyo kutambulika kimataifa.

Aitha Mgeni rasmi katika sherehe hizo Dkt Ashantu Kijaji aliyewakilishwa na Mh. Bi Amina Khamis Shaban ameitaka bodi hiyo kusimamia miendendo ya wanataaluma ikiwemo kuchukua hatua za kuwafutia usajili wale wote wanaokiuka taratibu na mienendo ya taaluma.

“Ili kuthibiti mienendo ya kimaadili ya wataalam wenu, ni lazima watu wote wanaofanya kazi za ununuzi na ugfavi nchini, wawe wamesajiliwa na bodi kwa mujinu wa sheria” alisema Amina Shaban.

Vilevile amewahasa wahitimu kutumia fulsa ya utaalamu wao kwa manufaa ya taifa na kusaidia kupunguza hasara kwa taifa zinazoweza kujitokeza kutokana na ununuzi na ugavi, pia wasitumie fulsa ya elimu waliyopata kwa ajili ya kuchukua rushwa ili kufanikisha ubadhirifu utakao ipa serikali hasara.

Aliongeza kuwa “mtu yeyote atakayebainika kuingiza hasara au kupokea rushwa kutokana na ofisi, cheo hama nafasi aliyonayo tutamfukuza na kumfungulia mashitaka, serikali ya awamu ya tano haitamvumilia yeyote atakayefanya kosa hilo”.

Hata  hivyo amewataka wahitimu hao kujiendeleza na wasibweteke kwa elimu waliyopata ila wanatakwia kujiendeleza na kuwa wabunifu kutokana na mabadiriko ya teknolojia  na kimfumo yanayobadirika kila siku ili mambo mapya yasiwapite bila kujua.

Post a Comment

 
Top