0
Nchi kadhaa duniani zimekiwa na uhuru kwa raia wake kqa jinsia zote kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa na mashine za umeme na hata zile zilizoonekana mtumiaji wake akitakiwa kuwa mtu mwenye nguvu.

PHOTO: Mwanamke wa Saudia katika kampeni ya
kukaidi wanawake kutoendesha magari
Hali hiyo imepelekea baadho ya nchi kuzuia matumizi ya baadhi ya vifaa kama magari kutumiwa baadhi ya watu ambao ni wanaume na wanawake wakiachwa ikionesha kubagua kada hiyo.

Kwa mara ya kwanza hivi karibuni Saudi Arabia itawaruhusu wanawake kuendesha magari kwa mujibu wa amri iliyotolewa na mfalme wa nchi hiyo.
Vyombo vya habari vimeripoti Jumanne kuhusu amri hiyo ya kifalme ambayo inataka leseni za kuendesha magari zitolewe kwa wote wanaume na wanawake.
Saudi Arabia hivi sasa ni nchi pekee ambapo inawazuia wanawake kuendesha magari. Shirika la habari la Saudi Arabia -SPA limeripoti kuwa amri hiyo itaanza kutumika rasmi mwezi Juni mwaka 2018

Source: VOA

Post a Comment

 
Top