ARUSHA.
Taasisi binafsi
kutoka nchini Marekani ya #Wheelchair Foundation iliyopo katika jimbo la Carifonia imetoa viti takribani 490
nchini kusaidia watanzania wenye ulemavu waweze kumudu kujongea kwa urahisi na
kuendesha maisha yao.
Katika hafla fupi iliyofanyika
kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha ambapo viti 60 vya walemavu
mbalimbali kutoka jiji la Arusha vilikabidhiwa hapo jana, mkuu wa wilaya Fabian
Daqqaro amewasshukuru wahisani hao kwa moyo wao na kuwataka wananchi waliopata
vitu hivyo kuvitunza katika matumizi yao ya kila siku ili viweze kuwa msaada
katika shuguli zao za maisha ya kila siku.
KUIJALI JAMII KWA DHATI.
PHOTO: Sehemu ya viti vyenye magurudumu
ambavyo vimetolewa kwa wananchi wa jiji la Arusha mapema jana.
|
PHOTO: Wananchi wakifuatilia majina yao kwa
afisa (jina halikupatikana) aliyekuwa
akisoma majina wakati wakukabidhi
viti kwa walengwa.
|
PHOTO: Mmoja wa wahisani kutoka #Wheelchairfoundation akibadilishana mawazo na mwananchi aliyepata msaada wa kiti kwa
niaba ya mwanae.
|
PHOTO: Baaadhi ya vijana wadogo walemavu
wakiwa wamekaa
kwenye viti vyao mara baada ya kukabidhiwa.
|
PHOTO: Mbali na viti hivyo kumekuwepo na
aina tofauti ya viti
kama hiki
cha walemavu maalum ambao viti vyao vimekuwa
ni tofauti
na vingine.
|
PHOTO: Wahisani kutoka Wheelchair
Foundation kutoka
marekani
wakiwa na mmoja wa wananchi aliyepewa msaada wa
kiti mapema
hapo jana.
|
Post a Comment