0
PROFILE PHOTO: Rais Dr. John Pombe Magufuri. 
Rais Dr. John Magufuli amezitaka Asasi za Kiraia (NGO’s) kufungua shule zao ili wanafunzi wanaopata mimba wakiwa masomoni basi waweze kusoma katika shule hizo kama kweli zinawapenda wanafunzi hao.

Rais ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.

“Si kwamba nawachukia wenye mimba, hata kwa bahati mbaya akapata mimba, kama hizo NGO zinawatetea sana, zifungue shule za wenye mimba, kwa sababu zinawapenda wenye mimba, wafungue shule zao,”

Amesema hata hao wanaofanya makongamano ya kuhamasisha watu wapate mimba wafungue shule zao kwa ajili ya wanafunzi hao.

Aliongeza kuwa "Haiwezekani fedha za walipa kodi, Sh 17 bilioni kila mwaka za kusomesha watoto wetu, kwenda kusomesha wakinamama, wazunguke, waimbe, waseme nini mimi ndiyo Rais, huo ndio ukweli"

Amesema tatizo si wanaopata mimba, kwani wapo waliopata matatizo, kama kuugua kwa muda mrefu wakashindwa kwenda shule lakini ulianzishwa mpango maalum wa kuwasomesha katika mfumo usio rasmi.



Post a Comment

 
Top