ROMBO.
Waumini
wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji walipokuwa wakibatizwa katika mto
Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza
majini.
Mkuu wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio
hilo lililotokea, Julai 16 saa sita mchana. Ubatizo huo ulifanyika kwenye kina
kirefu cha mto huo.
PHOTO: Haina uhusiano na habari hii. |
Amesema
wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha mapepo alimtumbukiza
mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.
Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na kuwasababishia kifo.
Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment