PWANI.
Ikiwa na
ziara ya siku tatu mkoani Pwani Rais John Magufuri akiwa kwenye mkoani pwani
kwa ziara ya siku tatu leo amefanya ziara kwenye kiwanda cha uzalishaji wa
Viududu kilichopo kibaha mkoa wa pwani.
PHOTO: Balozi wa Cuba nchini Prof. Lucas Domingo Hernandez akipokelwa na
Meneja Mkuu wa muda wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu Samwel Mziray.
|
PHOTO:
Balozi wa Cuba Lucas Domingo (kulia) akiteta jambo na waziri wa viwanda Mwijage
wakati wakimsubili Rais Magufuri kufika katika kiwanda hicho.
|
PHOTO: Rais John Pombe Magufuri akilakiwa
na Waziri wa viwanda na biashara Mwaijage alipowasili, kulia ni balozi wa Cuba
nchini Lucas.
|
PHOTO: Wafanyakazi wa Kiwanda cha
kuzalisha viualishe wakinywa dawa inayozalishwa kuzuia na kuua Mbu mbele ya
Rais ili kuonyesha kutokuwepo kwa madhara ikinywewa.
|
HABARI KWA UNDANI.
Katika ziara hiyo ambayo baadhi ya
wananchi hawakuitarajia, imeelezwa na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho
kuwa na tija kwao kutokana na hapo nyuma kuwepo kwa uzolotaji wa kununuliwa kwa
dawa inayozalishwa kutoka kiwwndani hapo.
Mara baada ya Rais
Magufuri kuzuru kiwanda hicho alitoa nafasi kwa Mkurugenzi wa shirika la
maendeleo la Taifa NDC ambao ndiyo wasimamizi wa kiwanda hicho kinachosimamiwa
na serikali pamoja na serikali ya Cuba mkurugenzi huyo ambaye jina
halikupatikana mapema alishindwa kutosheleza majibu kwa Rais pale alipoulizwa
kuhusu uzalishaji kiasi gani kwa mwaka ambapo alishindwa na badae Samweli
Mziray ambaye ni Meneja Mkuu wa muda akajitosa kumsaidia.
Mziray amemwambia
Rais kuwa uzalishaji wa dawa hiyo umedumaa kutokana na wizara ya Afya ambayo
ndiyo ilikuwa mdau mkubwa kununua dawa hiyo na kuisambaza, kushindwa kufanya
hivyo hali inayopelekea kupunguza uzalishaji ili kuepuka dawa nyingi kuharibika
ikiwa haijatoka kiwandani.
Hata hivyo Rais
Magufuri ameitaka wizara ya Afya na serikali kwa wilaya zote nchini kuanza
mchakato wa kuagiza Viualishi ili kuisambaza nchibi kote na kutokomeza mbu na
vizazi vyake.
Naye balozi wa
Cuba nchini amempongeza Rais Magufuri kwa kusimama imara na kuahidi serikali ya
cuba ipo bega kwa bega na itaendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada za
kuinua uchumi katika nyanja mbalimbali.
Post a Comment