0
DAR ES SALAAM.
Rais John Pombe Magufuri amekabidhiwa ripoti ya pili ya tathimini ya uchotwaji wa rasilimali ya nchi inayopatikana kwenye mchanga/Makemikia wa madini ikulu leo jijini Dar Es Salaam.

Mara baada ya sala kutoka kwa viongozi wa dini, wasanii waliounda kundi la pamoja la Tanzania All Star na kuimba wimbo wa Tanzania yetu waliimba.



Ukiwa na ng'ombe na mchungaji akawa anakwambia ng'ombe wako anatoa lita moja ika wewe siku ukiamua kwenda kuhakikisha kuwa ni kweli anatoa lita moja inaonekana umefanya makosa,  hii ni haki?


Katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, amesema kamati hii ya pili iliteuliwa na Rais ambapo jukumu kubwa lilikuwa kutizama mikataba ya kisheria na kuangalia adidu za rejea ambazo kamati ilikabidhiwa ili kuangalia tathimini ya madini yaliyokuwayakisafirishwa nje.

Adidu hizo ilikuwa kuweza kuangalia jinsi gani kuna ufanisi wa kuweza kuzuia upotevu wa fedha za serikali, pia kamati kuangalia kama serikali inapata kodi, kamati kuchunguza tathimini kutokana na mahabara zinazotumika ili kuona kama kuna upotevu wa maliasili.


Kamati hiyo iliweza kufanya uchunguzi ni makontena mangapi yalisafirishwa kutoka mwaka 1998 mpaka mwaka huu 2017, kuangalia jinsi gani nchi inaweza kufunga mtambo wa kuchanjua makemikia hapa hapa nchini lakini pia wataalam wa masuala ya madini waweze kutumika ili kulinda rasilimali za madini. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo Nehemiah Eliachim Osolo amesema kamati imefanya kazi mbalimbali zilizohusu makemikia hayo huku ikitembelea machimbo kadhaa ya madini pia bandari ya Dar Es Salaam na ofisi nyingine zilizopewa kipaumbele kuhusiana na nafasi ya kamati ilivyoamua.

Thamani ya madini yaliyopatikana kwenge makontena zaidi ya 44000  ni kiasi cha shs trilion 132.56.

Akizungumza kwa hisia huku akionyesha kuumizwa na hali ilivyo kwa viongozi wa serikali walikuwepo madarani kushindwa kusimamia rasilimali za nchi wakati wa kukabidhiwa ripoti hiyo,  Rais John Pombe Magufuri amesema, "mara ngapi mmachinga au mwenye kaduka kadogo dogo akifanya biashara bila kodi mnamfukuza na kumfunga ila hawa wenye makampuni makubwa na wanaotuibia hawaguswi".

Vilevile amegusia uwepo wa wasomi ambao wanashindwa kutumia elimu yao kwa manufaa ya nchi na kusema kuwa "kusoma  kwako hakuna tija endapo elimu yako haina faida kwa wananchi, kuna mmoja tumemshika akiwa anafanya fojare eti kwa sababu aliye juu yake ni mpale akitarajia atamsaidia, TUMEMKAMATA"

Na wale wote waliohusika na kufanya haya madudu naomba vyombo vya dola vifanye kazi yake ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Vita hii ni kubwa kuliko hata vita ya kupigana, kupitia Prof. Kabudi na wanasheria wengine naomba muunde muswada wa sheria ili muupeleke bungeni upitishwe hata ikiwezekana bunge likae hata wiki ili mradi sheria hii ipitishwe haraka. 

Katuka hatua nyingine Rais amewatahadhalisha wabunge wakorofi ambao wamekuwa wakileta sintofaham katika mijadala ndani ya vikao vya bunge na kumwambia spika, kazi anayofanya kuwapa kalipio kali ikiwemo na kuwafukuza bungeni.

UPDATES:
kampuni ya ACACIA imekubali kufanya mazungumzo kutokana na  kile Rais alichosema "wakiwa tayari" hali iyo imetokana na ripoti ya kamati na maamuzi yaliyotolewa hii leo.

Pamoja na hilo kampuni hiyo imepinga ripoti hiyo na kusema haina ukweli wowote na haina tofauti na ile ya kwanza iliyowasilishwa wiki tatu zilizopita. 

Post a Comment

 
Top