0
PHOTO: Mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze.
Imefahamika kuwa unapompa mwalimu malipo ya fedha mara baada ya matokeo kunamuongezea ufanisi unaotokana na nafasi, muda wake aliotumia kumfanya mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo. Hii imefahamika kupitia majaribio yaliyofanywa na shirika la Twaweza kwa kushirikiana na Tume ya sayansi na Teknolojia na shirika la IPA kwa utafiti uliofanywa kwa miaka miwili.


PHOTO: Wanachuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma waliohudhulia mjadala na sherehr za kuwazawadia walimu bahshishi.

PHOTO: Mmoja kati ya walimu waliopokea tuzo, Mwalimu Rukia Mbiro akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs 1,256,577 kutoka kwa Waziri wan chi ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene.

PHOTO: Kushoto ni Mp Zitto Kabwe akisoma moja ya kijarida cha Twaweza, katika na kushoto ni wabunge waliohudhulia sherehe na mjadala huo.


PHOTO: Waziri wan chi ofisi ya Rais George Simbachawene akiongea wakati wa kutoa hotuba yake juu ya Utafiti huo wa Twaweza ulioshirikisha Taasisi ya Sayansi na Teknolojia na IPA.

PHOTO: Baadhi ya walimu kutoka shule za jijini Dar Es Salaam pamoja na viongozi wa serkali za mtaa waliokuwepo katika sherehe hizo.

PHOTO: Waziri wan chi ofisi ya Rais George Simbachawene akiongea wakati wa kutoa hotuba yake juu ya Utafiti huo wa Twaweza kwa walimu wabunge na wageni mbalimbali.

PHOTO: Baadhi ya walimu na wageni waliohudhulia mjadala na sherehe.


PHOTO: Mbunge  wa Kigoma Mjini Zuberi Zitto Kabwe akitoa neno kuhusu mfumo wa Elimu nchini juu ya bahshishi kwa walimu katika sherehe hizo

PHOTO: Viongozi, walimu wakifurahia jambo wakati Mbunge Zitto Kabwe (Picha juu) alipokuwa akiongea.

PHOTO: Picha ya pamoja kwa walimu, wabunge na viongozi mbalimbali wakiwemo Twaweza katika ukumbi kwa hazina Kambarage -Treasury Square mjini Dodoma.



DODOMA.
Katika hotuba yake kwenye sherehe fupi ya kuwapatia zawadi walimu kadhaa waliofanya vizuri kutoka mikoa iliyofanyiwa majaribio,Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene amesem mpango huo wa kuwalipa walimu baada ya matokeo ni mzuri na unaleta thamani na tija kwa walimu na serikali inatambua mchango wa taasisi binafsi ikiwemo Twaweza nyanja ya Elimu hasa katika majawabu ya kuinua kiwango cha Elimu nchini.

Aliongeza kuwa kama matokea ya kujifunza kwa walimu wanaofundisha darasa la kwanza, pili na la tatu kufanya vizuri katika kufaulisha wanafunzi, motisha hiyo inayotolewa kwa walimu ni kweli inachochea kuleta matokeo chanya na kuleta mjadara mpana ambao unaleta matokeo mazuri zaidi.

“sikatai kabisa kwamba kama motisha ikitolewa inaweza ikawa ni kichocheo kwa walimu kufanya vizuri lakini pia inaleta kichocheo kwa wanafunzi kujifunza, sisi washiriki na wadau mbalimbali wa elimu hapa nchini tunapaswa kutafakali na kuangalia namna bora ya kutekeleza mpango kama huu nchi nzima” alisema George Simbachawene.

Hata hivyo Waziri amesema Serikali kwa sasa inatoa fedha nyingi kwa sekta ya elimu na kuweza kugharimia sehemu kubwa ambayo leo ndiyo hiyo watu wanayoiita Elimu bure, “kwa mwezi mmoja kwa sasa serikali inatoa kiasi cha shilingi 25.5bilioni kuweza kwa ajili ya maeneo yote muhimu” pia amewataka Twaweza kufanya utafiti huo nchi nzima ili kuweka wigo mpana kwa walimu kujitathimini kupitia mpango huo wa Kiu ya Kujifunza ambapo utawafanya walimu wengi kujituma ambapo nafasi ya kufaulu itaongezeka.

Matokeo ya utafiti huo unaojulikana kama KiuFunza ambao majaribio yake yamefanyika katika shule 200 zilizoko kwenye wilaya 21 nchini ni moja ya tafiti za aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo baadhi ya wabunge, viongozi kutoka wizara ya TAMISEMI na wananchi wengine walihudhulia sherehe hizo zilizofanyika  katika ukumbi wa Hazina Kambarage mjini Dodoma.

Twaweza imeweza kuwazawadia walimu 788 wanaofundisha madarasa ya I,II na III na walimu wakuu 135 kwa mwaka uliopita wa 2016 ikiwa ni jumla ya shs 251,827,040,000, pia mgawanyo mwingine ulienda kwa viongozi wengine wa kata na serikali.

Taasisi hiyo imeamua kujikita katika utoaji wa motisha kwa walimu ikiwa ni moja ya ushaidi kutoka maeneo mbalimbali duniani kuwa utolewaji wa motisha unaonyesha kuwahamisisha walimu kuongeza jitihada na kuleta matokeo chanya ya kujifunza.

Mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyekuze anasema “Japokuwa kujifunza kunachangiwa na mambo mengi, tumeonesha kupitia utafiri wa kisayansi kuwa kuchanganya motisha na uwajibikaji kunaweza kuleta matokeo mazuri ya kujifunza kwa watoto, tuna ushahidi thabiti wa kile kinachoweza kufanyika na kuwa na uhakika kuwa tukifanya hicho watoto watajifunza”

Hata hivyo Twaweza inafanya kazi kwa lengo la kuwawezesha watoto kujifunza, wananchi kuwa na utayari wa kuleta mabadiriko huku serikali kuwa wazi zaidi na sikivu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, vilevile mpango huo uliofanyika katika kuwapanga wanafunzi kwenye moja kati ya makundi 10 kitaifa kulingana na uwezo wao uliotokana na majaribio yam waka uliopita.


Post a Comment

 
Top