0
PHOTO: Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi
Taifa na Mbunge Abdallah Majura. 
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa na mjumbe wa mkutano  mkuu wa chama cha Mapinduzi NEC Abdallah Majura Burembo amefanya mkutano na wanachama, wajumbe, viongozi, madiwani, makatibu na viongozi wa serikali ambao ni wanachama wa chama cha mapinduzi mjini Dodoma kwenye ukumbi wa makao makuu ya CCM mjini Dodoma mapema leo.


PHOTO: Katibu wa CCM Dodoma mjini Jamila akimkaribisha mwenyekiti na Mbunge Burembo katika mkutano huo.

PHOTO: Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiongea na wanachama na viongozi wa CCM Manispaa ya Dodoma, ambapo ameahidi kuwawekea TV kubwa katika uwanja wa Nyerere Square.

PHOTO: Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme akitoa salamu kwa wanachama na kuwataka kuwa na imani na serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuri.

PHOTO: Mwenyekiti wa CCM Dodoma mjini Paul Luhamo, akiongea na hadhira juu ya Rais kuivunja cda kisha kusoma TAMKO rasmi la kumshukuru Rais Magufuri kwa kuvunja cda.

PHOTO: Baadhi ya wanachama na viongzi wa CCM manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuioya ya wazazi Taifa na Mbunge Abdallah Burembo (hayupo pichani)


PHOTO: Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi na Mbunge Abdallah Majura (katikati) Burembo akisalimia na mzee Lusinde (kulia), akiwapa maelezo ya kina viongozi juu ya uchaguzi wa ndani ya chama.




DODOMA.
Katika mkutano huo uliohudhuliwa na viongozi hao umelenga kuwaweka wanachama kujitoa kuwania nafasi za uongozi kuanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa na kukukitumikia chama pamoja na katika mabadiriko makubwa yanayofanywa ndani ya chama cha mapinduzi kwa sasa.

Mh. Burembo ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliteuliwa na Rais John Pombe Magufuri ameongea na viongozi mbalimbali waliofika kumsikiliza ikiwa ni mojawapo ya ziara yake nchini na kwa manispaa ya Dodoma ikiwa ni wilaya ya mwisho kumalizia ziara mkoani Dodoma.

Kupitia mkutano huo amewataka madiwani waliopo manispaa ya Dodoma kujitathimini kwa nini kunakuwa na migogoro kati yao na ambayo ndiyo chanzo cha matatizo yanayoweza kuleta mtifuano na kusababisha wapinzani wa CCM kupata upenyo wa kuinga kupitia migogoro hiyo ya ndani ya chama, “tangu uchaguzi kumalizika hakuna kiongozi ambaye aliwahi kumtembelea kiongozi mwenzake aliye chini hama juu yake, na kama yupo basi asimame mbingu imuone” alisema Burembo.

Pia amesisitiza umoja na ushirikiano ndani ya chama ili kujenga msingi na imaya ya chama kwa wakati ujao, “haiwezekani Rais apokelewe na Meya wa upinzani haiwezekani hata kidogo, tunayo nafasi na muda wa kuweka misingi imara kwa wakati ujao sasa ili hili lisitokee”

Kutokana na baadhi ya wanachama kupendekeza wagombea wao katika nafasi za uongozi Mh. Burembo alisema “kuna watu wanasema nina mtu wangu, mtu wako ni mkeo tu ambaye mnaweza kupanga naye maze mtoto, lakini hata huyo mtoto lakini hata kumbuka hata huyo mtoto akizaliwa siyo wako ni mali ya serikali, ndani ya CCM mpya hakuna mtu wangu”

Amewata viongozi kujitambua kuwa wao ni jalala, maana kila mtu anakuja kwako kutaka huduma na hitaji lililo juu hama chini yako na inakupasa ufanye jitihada kumsaidia.

Naye mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme akitoa salamu zake kwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi na Mbunge Burembo, amemshukuru Rais na mwenyekiti wa CCM John Magufuri kwa uhamuzi mujarabu wa kulindoa dudu lililowaumiza wananchi ‘CDA’ na kusema hatua hiyo inampa nguvu kutokana na malalamiko lukuki aliyokuwa anapoke kila uchao.

Vilevile mbunge wa Dodoma Anthony Mavunde pia amemshukuru Rais kwa kutekeleza moja ya ahadi zake za kuivunja cda na ambapo katika kipindi cha uchaguzi alionekana kuwa mmoja wa viongozi “waliosadikika” kuwa upande wa cda hivyo baadhi ya wananchi kumuona ni kibaraka wa udhalimu uliokuwa unafanywa na cda.

Post a Comment

 
Top