PHOTO: Mkuu wa mkoa wa
Mbeya Amosi Makala (aliyeshika kioaza sauti) akiongea wakati wa mkutano na
wananchi alipokuwa akisikiliza kero zao, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya
Paul Ntinika.
|
PHOTO: Mmoja wa wananchi wa
mkoa Mbeya akitoa moja ya kero anazokumbana nazo jijini humo.
|
Na Marry Mwakibete –MBEYA.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya
Amosi Makala amewaagiza viongozi wa jiji la Mbeya wakiwemo wakuu wa Wilaya,
Sumatra, Jeshi la Polisi, viongozi wa Bajaj, Daladala, Bodaboda kuweza kukutana
kuweka mikakati itakayoweza kuepusha msongamano pamoja na ajali katika jiji la
Mbeya.
Akizingumza katika
mkutano wa viongozi wa mkoa wa Mbeya mkuu huyo wa Mkoa ameomba ushirikiano wa
kutosha kwa viongozi, watendaji na wananchi kuunga mkono jitihada hizo ili
kuweza kufikia maendeleo yasiyokuwa na vikwazo sehemu mbalimbali na kuweza
kuokoa muda.
Akizungumza katika
mkutano wa kusikiliza kero za wananchi kupitia utaratibu aliojiwekea ili
kuwasikiliza pia ameahidi kuitisha mkutano muda wowote na wenyeviti, makatibu
wa mabaraza ya ardhi ili kuweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuondoa
matatizo waliyonayo wananchi.
Post a Comment