Na. Mary Mwakibete. MBEYA.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Gabriel Makalla amefanya ukagua kwenye eneo ambako ujenzi wa meli tatu
unaofanywa katika Bandari ya Kyera ambapo amejionea kukamilika kwa moja ya
meli hizo ambayo inategemewa kukabidhiwa mwisho wa mwezi huu.
![]() |
PHOTO: Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katikati akiwa na viongozi kadhaa wa mkoa na wataalam wanaofanya ujenzi wa meli tatu katika Bandari ya Kyera
mkoani Mbeya.
|
Ujenzi wa meli hizo tatu unaofanywa katika bandari ya
Kyera mkoani Mbeya unatekeleza malengo ya serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuri katika maendeleo ya sekta ya uchumi
pia kuendeleza uchumi kwa kanda ya nyanda za juu kusini.
Katika ukaguzi huo mkuu huyo
wa mkoa amesema ujenzi huo wa meli unakwenda sambamba na uhusiano wa nchi
zinazopakana na Tanzania na unakusudiwa kukuza mahusiano mazuri yaliyopo ikiwa
ni biashara na maendeleo ya haraka kwa nchi hizo jirani kama Malawi wakati
uhusiano ukiwa ni mzuri kuliko wakati wowote.
Aitha ameitaka serikali za
mkoa wa Mbeya, Njombe na Ruvuma kuboresha barabara zote zinazoingia kwenye
bandari hiyo ili kuweka wepesi wa usafiri kuingia na kutoka katika meli hizo na
wakati huo huo amewaomba wafanyabiashara na makampuni kujiandaa kutumia
meli mbili za mizigo na moja itakayobeba abiria kwa ajili ya usafiri na
usafirishaji wa bidhaa mbali kwa wananchi wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine RC
Makalla amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kijamii zinazosababisha
kuongezeka na kuharibika kwa mazingira fukwe, kuchimba mchanga na kukata magogo
kwenye eneo la bandari hali inayopelekea kupunguza kina cha maji na kuongeza
tope bandarini.
Post a Comment