PROFILE PHOTO: Rais Magufuri Pombe Magufuri. |
DAR ES SALAAM.
Serikali imechukua uamuzi wa kumfukuza mwakilishi
mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) ambaye anatuhumiwa
kuwa kikwazo katika shughuli za shirika hilo nchini Tanzania.
Waziri wa mambo ya nje Dr. Augustine
Maiga amesema Awa Dabo ambaye ni raia Gambia amekuwa na mahusiano yenye mvutano
na wenzake wa ofisi moja kutoka kwenye shirika hilo la Umoja wa Mataifa na kwa
hiyo ametakiwa kuondoka nchini Tanzania mara moja.
Bi Dabo, ambaye tayari amekwishaondoka
hapa nchini, alipewa muda wa saa 24 awe ameshaondoka nchini na taarifa ya
Wizara ya mambo ya nje inasema kuwa usimamizi mkali wa bi Awa Dabo ulizuia
shughuli ya shirika hilo hapa nchini kutotendeka vizuri.
Hata hivyo serikali imeomba UNDP kuwakumbusha wafanyakazi wake
kwamba kipaumbele chao cha kwanza ni kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali
ili kufikia malengo yake ya maendeleo endelevu yenye tija kwa nchi.
Kupitia taarifa ya wizara ya mambo ya nje ilisema kuwa"Uwepo wake ulikuwa kikwazo kwa juhudi za maendeleo ya nchi,"
PROFILE PHOTO: Rais Magufuri akisalimia na aliyekuwa mwakilishi wa UNDP nchini Awa Dabo.
Post a Comment