0
PHOTO: Mkurugenzi wa mtendaji JUKATA Hebron Mwakagenda 
DAR ES SALAA.
Jukwaa la katiba nchini JUKATA limetoa pongezi na pendekezo la kwa waziri mpya wa wizara inayohusika na katiba na sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi pamoja na mapendekezo ya kukamilisha mchakato wa katiba uliokuwa ukiendelea ukiwa chini ya mwenyekiti na jaji mstaafu na aliyewahi kuwa waziri mkuu hapa nchini Joseph Sinde Warioba.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya JUKATA jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa mtendaji Hebron Mwakagenda amesema kuwa Jukwaa la katiba Tanzania linaendelea kufuatilia kwa umakini mkubwa namna serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza masuala muhimu ya kitaifa chini ya uongozi wa Mhe. Dkt John Pombe Magufuri.

“tumebaini utekelezaji duni wa bajeti yam waka 2016/2017 katika miradi ya maendeleo, ambapo Jukata inasikitishwa na taarifa za serikali kwamba hadi mwezi Machi 2017, miezi mitatu kabla ya utekelezaji wa bajeti kukamilika, serikali imeweza kupeleka shs trilion3.5, hivyo itakuwa ni ajabu kama serikali italeta bajeti ya 2017/2018 yenye sura kama hii ambayo haitekelezeki na kamwe ndoto ya Tanzania ya viwanda itabaki kuwa ndoto kama maana halisi ya neno ndoto” alisema Mwakagenda.


Serikali itoe taarifa rasmi kwenye gazeti la serikali kuhainisha mchakato wa katiba kuwa hupo hai na utaendele tena ili kupata Katiba mpya, hata hivyo TODAYS NEWS tumepata taarifa zaidi na tumekuwekea hii hapa chini katika HABARI VIDEO  …


Post a Comment

 
Top