0
Msanii na mwigizaji Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya mihadarati, amedai maisha yake yapo hatarini kutokana na kutishiwa maisha na watu wasiojulikana mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha chadema. 


 Na Joseph Ngilisho -ARUSHA
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Arusha wakati alipomtembelea mbunge wa Arusha mjini God bless  Lema kwa lengo la kumpa pole ambapo alisema hali hiyo imemfanya ajiongeze zaidi kwa kujiimarishia jeshi lake la  ulinzi yeye na mama yake na kudai kwamba hatishiki na vitisho hivyo na amejipanga kukabiliana navyo kwa hali yoyote ile na yupo tayari kwa mapambano. 

Aidha aliongeza kuwa tangu ahamie chadema anajisikia amani kwani mzigo aliokuwa nao ameutua na ndio maana hata afya yake imenawili, amenenepa. "Tangu nihamie chadema Moyo wangu una amani nahisi nimeutua mzigo mzito sana, nimenawili ndo maana unaona nimenenepa" Alisema Wema

Akizungumzia suala la wasanii wenzake kubeza uamuzi wake wa kuhamia chama cha chadema, alisema hana muda wa kujibizana na wapumbavu,  huo ni uamuzi wake na aliahidi kufanya mambo makubwa akiwa chadema kwa kutumia nafasi yake ya usanii. Kwa upande wa suala la mama yake kukamatwa na polisi akidaiwa kutapeli mamilioni ya fedha kutoka kwa mfanyabiashara Alex Msama,Wema bila kufafanua alisema huo ni mwendelezo ya mengi yatakayotokea katika kipindi hiki. 

Hata hivyo alidai kuwa suala hilo halina ukweli wowote kwa sababu yalikuwa ni makubaliano yao na kulihusisha suala hilo na masuala ya kisiasa, ukizingatia kuwa hivi karibuni pia mama yake alivamiwa na kundi la watu wasiofahamika na kuanza kuponda mawe mengi juu ya nyumba yake anayoishi peke yake. 

"Kiukwe mama yangu sio tapeli hiyo nyumba inayodaiwa kuwa amemtapeli mamilioni, Alex Msama sio kweli kwani walikuwa kwenye makubaliano yao na hakuna kesi ya msingi hayo ni mambo ya kisias tu na tunayatarajia mengi" Alisema Wema. 

PHOTO: Wema Sepetu akiwa na mdau wa Chadema Ndaro Bwire.

Wakati huo huo, Wema amedai kukamatwa na kushikiliwa kwa zaidi ya dakika 20 na maofisa wa uhamiaji katika mpaka wa Namanga wakati akitokea nchini Kenya akitumia gari binafsi lenye usajili wa nchi hiyo alilokuwa amekodisha akiwa jijini Nairobi .

Alisema maofisa hao baada ya kulikamata gari hilo walimhusisha na yeye bila kufafanua sababu za msingi wakati yeye alikuwa amekodisha kwa ajili ya safari zake na kumfanya asote mpakani hapo  kwa zaidi ya dakika 20 na hivyo kudai kuwa huo ni mpango wa kuendelea kumdhibiti. 

Hata hivyo alisema anajivunia kuingia chadema akidai chama hicho kina umoja na ushirikiano mzuri na kina wanasheria mahiri ambao anaamini watamsaidia.  Vilevile alisema anafikiria kuhama nchi iwapo atamaliza salama kesi yake ya dawa za kulevya inayomkabili kwani amesitishwa  na mambo anayofanyiwa ndani ya nchi yake.

Kwa upande wake mbunge Lema alimkaribisha kwa kishindo Wem na kumtaka aondoe ubishoo kwani awapo chadema atarajie mengi kumkuta ikiwemo kulala polisi. "Wema karibu sana chadema ila uwe ngangali mambo ya ubishoo huku hakuna, uwe tayari kulala polisi muda wowote" Alimwosia  Lema. 

Post a Comment

 
Top