Mkuu wa mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo amezindua mfumo wa kasi wa kampuni ya mawasiliano wa TTCL
unaojulikana kama 4G LTE kwa mara ya kwanza mkoani Arusha ikiwa ni sehemu
mojawapo ya kuongeza ufanisi, gharama nafuu na huduma kwa wigo mpana wa kampuni
hiyo kongwe nchini, ambapo katika uzinduzi huo ulifanyika mapema leo asubuhi
ilikuwa ni zawadi kwa mwaka mpya 2017 kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na kwa Taifa
kwa ujumla.
![]() |
| PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akionyesha ishara ya T kama uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE mkoani humo ishara hiyo hutumiwa na kampuni ya simu ya TTCL kuzungumizia kizazi cha teknilojia. |
![]() |
PHOTO: Baadhi wa wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya TTCL mkoani
Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha
Gambo katikati waliokaa.
|
ARUSHA.
Uzinduzi wa teknolojia
hii 4G LTE ni moja kati ya mipango mkakati ulio katika biashara wa miaka mitatu
unaolenga kupeleka huduma mpya sokoni na kuongeza tija katika uwajibikaji na
huduma kwa wateja ikiwa ni mpango kabambe wa kuboresha miundo mbinu ya kampuni
na kuweza kuimarisha mtandao wa simu na data wa kampuni hiyo ambayo ni mhimili
wa mawasiliano hapa nchini.
Mkurugenzi wa biashara
wa TTCL kanda ya kaskazini Simon Marwa anasema uzindizi wa 4G LTE umeongeza
wigo wa mikoa ambayo itakuwa ikipata huduma hiyo ikiwemo, Tanga, Morogoro,
Mwanza, Mbeya, Dodoma, Pwani, Dar Es Salaam na kwa sasa Arusha pamoja na visiw
vya Unguja na Pemba. “kampuni ya TTCL imepitia mawimbi mengi kiasi cha
kuwakwaza wateja wetu na wananchi kwa ujumla, naomba kutumia fulsa hii
kuwahakikishia kuwa tumevuka salama mawimbi ambayo yametuimarisha na sasa
tumekuwa thabiti zaidi.” Simon Marwa.
Aidha Marwa ameuomba
uongozi wa mgeni rasmi Mrisho Gambo akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa, kuendeleza umoja katika vita ya kupambana na vitendo vya
hujuma vinavyofanywa na baadhi ya watu wenye nia mbaya dhidi ya mbinu
miundombimu ya kampuni hiyo ukiwemo mkongo wa Taifa wa MawasilianO.
Wakati huo huo mkuu wa
mkoawa Arusha aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo ameipongeza TTCL kwa
kuleta huduma hiyo mkoani Arusha ikiwa kwa sasa imekuja ikiwa ni mali ya
Watanzania kwa asilimia, ikiwa ni pamoja na mapato na faida yote inabaki hapa
nchini kwa sasa.
TTCL ndiyo imebeba
jukumu la kuwaunganisha wananchi kwa mawasiliano ya uhakikana inayobeba jukumu
la kufanikisha utendaji wa sekta ya mawasiliano pamoja na jukumu la kufanikisha
utendaji wa sekta nyingie zikiwemo shuguli za ulinzi na usalama wa nchi.
“Juhudi za Rais wetu mpendwa Mhe Dkt John Pombe Magufuri ambaye mara
zote anataka kuona mashirika ya umma yakiwa hai, yakitoa huduma kwa wananchi
pamoja na kujiendesha kwa faida kuweza kuchangia katika pato la taifa na ukuaji
wa sekta nyingine, hivyo kufanikisha mpango makakati wa Serikali ya awamu ya
tano wa kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda” alisema
Gambo.
Katika hatua nyingine
RC Gambo amewataka watendaji wa TTCL kuacha kuendelea kufanya kazi kwa
utaratibu wa kawaida na mazoea, bali
wabadilike ili kuleta mapinduzi, sura mpya na mtazamo mpya wa kampuni kwa
jamii. Amesema “kuweni
wabunifu, jifunzeni kwa wenzenu waliofanikiwa na hakikisheni kuwa wateja wenu
wanaridhika na huduma zenu huku wakiwa mabalozi wenu kwa wengine”



Post a Comment