FULL STORY:
Idadi kubwa ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wameripoti uhaba wa chakula katika maeneo wanayoishi. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 84 wameripoti uhaba wa chakula ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo ya mijini.
Idadi kubwa ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wameripoti uhaba wa chakula katika maeneo wanayoishi. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 84 wameripoti uhaba wa chakula ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo ya mijini.
DAR ES SALAAM
Zaidi ya nusu ya kaya za Tanzania (yaani
asilimia 69) zinahofia kuishiwa chakula. Aidha asilimia 51 ya kaya zimeripoti
kwamba hakukua na chakula cha kutosha kulisha kaya nzima, au mwanakaya
ameshinda na njaa kwa sababu hakuweza kupata chakula (asilimia 50).
Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika
muhtasari uitwao Uchungu wa njaa: Upungufu wa chakula
Tanzania. Muhtasari huu umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi,
utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia njia ya
simu.
Takwimu za muhtasari huu zimekusanywa
kutoka kwa wahojiwa 1,800 wa Tanzania bara (Zanzibar haikuhusishwa kwenye
matokeo haya) kati ya tarehe 14 na 26 mwezi wa tisa, 2016 na kutoka kwa
wahojiwa 1,610 kati ya tarehe 9 na 15 mwezi wa pili 2017.
Kwa mujibu wa wananchi wengi, uhakika wa
kupata chakula umepungua kati ya mwezi Septemba 2016 na Februai 2017: Mwezi wa
pili 2017, asilimia 65 ya wananchi walikuwa
na hofu ya kaya zao kukosa chakula cha kutosha ikilinganishwa na
asilimia 45 waliosema hivyo mwezi Septemba 2016.
Mwezi Februari 2017, asilimia 51 ya
wananchi waliripoti kwamba kuna
wakati hawakua na chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao katika
kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Kabla ya hapo, mnamo mwezi Septemba 2016,
asilimia 43 ya wananchi iliripoti kwamba hali kama hiyo iliwatokea katika
kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita.
Mwezi Februari 2017, asilimia 35 ya
wananchi waliripoti kuwa na mwanakaya angalau mmoja alieshinda na njaa siku nzima kwa sababu ya
kukosa chakula katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, hili ni
ongezeko kutoka asilimia 21 walioripoti kwamba hali hiyo iliwatokea katika
kipindi cha miezi sita tangu Aprili mpaka Septemba 2016.
![]() |
| Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji Twaweza |
Wahojiwa wa Sauti za Wananchi wameripoti
kwamba kwa wastani kilo moja ya mahindi inawagharimu shilingi 1,253. (Bei
zilizoripotiwa kwenye masoko ya ndani).
Upungufu na uhaba wa chakula unaoendelea
ni kielelezo cha hali ngumu ya maisha iliyopo na umasikini wa kipato. Jumla ya
watu nane kati ya kumi (asilimia 80) wameripoti kwamba kaya zao hazina kipato
cha kutosha kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa
Twaweza anasema: “Wananchi wamekumbwa vikali na upungufu
wa chakula. Tumepokea mwitikio wa serikali katika suala hili na tunaunga mkono
jitihada za kuzuia maafa makubwa.
Anaendelea kusema, “takwimu
zinaonesha kwamba wananchi bado wanaishi kwenye hali ngumu na wamejaa hofu ya
kukosa chakula. Jitihada za kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania yeyote anayelala
njaa zishike nafasi ya kwanza katika vipaumbele vyetu vya kitaifa.”
Kwa ujumla, wananchi hawana uhakika wa chakula lakini hali imezidi kuwa mbaya siku za karibuni

Post a Comment