Mkutano wa halmashauli
kuu ya chama cha mapinduzi NECulioanza hivi karibuni mjini Dodoma kwa kamati
kadhaa kukutana na kujadili ajenda muhimu pamoja na kupitisha maazimio ya
kuwafukuza baadhi ya wananchama wa CCM waliokwenda kinyume na kukisaliti chama.
DODOMA
![]() |
| M/kiti wa CCM JP Magufuri katkati akiongea. |
Mkutano huo umeendelea
jana na leo mjini humo ambapo kwa siku ya jana Rais na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi John Magufuri aliweza kuingia katika ukumbi ambako mkutano huo
unafanyika mapema kabla ya wajumbe wa mkutano huo wapatao 376 kuingia ukumbini,
hali inayokwenda kinyume na Itifaki ya uongozi.
Kutokana na hali hiyo
wajumbe wa mkutano huo ambao wengi walikuwa nje wakiongea na wengine kunywa
chai na kubadilishana maongezi walipewa
taarifa kuwa Mwenyekiti ameshaingia ukumbini
ndipo baadhi walionekana kutimua mbio na kuacha chai na wengine wakienda kwa
haraka kuingia ndani.
Wakati wa kuanza kwa
hotuba yake Magufuri alianza kwa kuwapiga viongozi wa chama hicho wa mikoa
ambao ni makatibu, wakati wa kumpitisha mgombea wa kiti cha urais hawakumpa
ushirikiano mwenyekiti aliyepita Jakaya Kikwete, bali kuna baaadhi ya wajumbe
wa NEC walionyesha hisia zao moja kwa moja kwa kuwa na imani na Edward Lowasa,
hivyo haoni tija kwa makatibu hao kuwepo katika vikao vya juu kwa sababu kuna
wenyeviti wao wanakuwepo.
Akitolea mfano wa
balaza la mawaziri ambalo hufanyika pasipo kuwepo kwa manaibu waziri wala
makatibu wakuu, lakini ushiriki wao hauathili vikao hivyo.
Pia aliongeza kwa kusisitiza
kuwa “wakati
wa mkutano kama huu uliopita walisimama na kumpinga mwenyekiti na makatibu
mlikuwepo, mbona hamkusimama kumpigania?, na bado watu wakaendelea kuimba wana Imani
na mtu fulani”

Post a Comment