0
Muwindaji haramu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na kuua na kuchukua pembe za ndovu nchin na ambaye pia alifahamika kama shetani wa wanyama amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.

PROFILE PHOTO: Shehena ya pembe za ndovu
ambazo zimechomwa moto hivi karibuni nchini kenya.
Boniface Metthew Maliango alikamatwa akiwa na pembe za ndovu 118 zenye thamani ya dola za Marekani 860,000 na kufunguliwa mashtaka, ambapomara kadhaa amekuwa akikwepa kukamatwa lakini alitiwa mbaroni mwezi Oktoba mwaka jana.
Hii ni hatua kubwa kwenye vita dhidi ya uwindaji haramu na ujangiri hapa nchini na Afrika mashariki ambapo wanyama pori kama tembo ambao wapo hatarini kutoweka kutokana na matukio kadhaa ya uwindaji haramu.
Wakati vita hii ikishika kasi hapa nchini na dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuhifadhi wanyama pori shirika la chakula duniani FAO limetoa wito kuwahifadhi na kuwatunza wanyama pori.
Source rfi

Post a Comment

 
Top