![]() |
| PROFILE PHOTO: Rais john Pombe Magufuri |
Akizungumza Ikulu jijini Dar es salaam, Magufuli amewashtumu baadhi ya wanahabari kuandika taarifa ambazo amezitaja kuwa ni za kichochezi.
“Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, be careful, watch, kama mnafikiri mna freedom ya namna hiyo, not to that extend,” alisema Rais Magufuli.
Rais ameonekana kukerwa na taarifa zilizoandikwa katika Magazeti zikionyesha kutishiwa bastola kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na Michezo Nape Nnauye hapo jana alipokuwa anataka kuongea na waandishi wa habari.
“Picha yote ya ukurasa wa kwanza ni ya mtu aliyefanya kosa moja, kana kwamba hiki kitendo kimefanywa na serikali au kinaungwa mkono na serikali,” aliongeza rais Magufuli.
Aidha, amemuagiza Waziri mpya wa Habariz Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrisson Mwakyembe kuhakikisha kuwa anachukua hatua pale ambapo mtangulizi wake alishindwa kufanya hivyo.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wanabahari kuandika Habari zilizo sahihi na za usawa ili kuepusha ripoti zinazoweza kuzua uchochezi.

Post a Comment