Maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani ambayo yanategemewa kuitimishwa kesho duniani kote
yanatarajiwa kuwashuhudia kinamama wakikusanyika pande zote za dunia ili
kuonyesha namna mwanamke anathamani na nafasi yake kutambuliwa katika nyanja
mbalimbali.
![]() |
Muuguzi kutoka
kitengo cha mahabara katika hospitali ya mount
meru Gladness John
akimsaidia Seif Omary kutoa damu kwa
ajili ya benki ya
damu jijini Arusha.
|
![]() |
PHOTO: Sr. Gladness John akihifadhi damu
iliyotoka
kwa mwananchi
aliyejitolea.
|
![]() |
PHOTO: Dr. Gembe kulia akimuhoji mmoja wa
wananchi waliofika kupima
Afya katika kiwanja
cha Sheikh Amri abeid Arusha, kushoto ni
Sr, Georgia swai,
wote kutoka Hopstali ya Mount Meru.
|
![]() |
Wakina mama wakiwa katika foleni
kuelekea kwenye kipimo cha Saratani.
|
PHOTO By; TODAYS PRODUCTION
ARUSHA.
Ikiwa kesho ndiyo
kilele chake maandalizi ya siku hii yamekuwa yakifanyika wiki moja nyuma kabala
ya siku yenyewe, jijini Arusha maandalizi yamekuwa yakifanyika kupitia hatua
mbalimbali ikiwemo kwa taasisi mbalimbali kutoa huduma na bidhaa mbalimbali katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mojawapo ni hospitali ya Meru iliweza kuto huduma mbalimbali kwa jamii ikiwa ni
kuwapima kinamama magonjwa ya Saratani ya Matiti na Mlango wa uzazi.
“Toka
tumeanza kutoa huduma hii tunaona mwitikio kwa kinamama ukiw ni mdogo kulingana
na matarajio yetu yalikuwa kuona kinamama wengi wakijitokeza lakini mpaka sasa
mwitikio ni mdogo, hivyo tunwaomba kinamama wengi wajitokeze kupata huduma hii
ambayo ni bure na inaendelea hata baada ya maadhimisho haya kuisha pale katika
hospitali ya mkoa ya Mount Meru kila siku isipokuwa Jumamosi na Jumapili tu.” Anasema
Sr. Georgia Swai.
Semina na Elimu juu ya
dalili na magonjwa hayo imekuwa ikitolewa sehemu mbalimbali kama Makanisani na
misikitini lakini bado mwamko umekuwa ni mdogo sana, hali hii inasababishwa na
baadhi ya kinamama kuwa na kazi nyingi ikiwemo biashara ba wengine kusuburi
ugonjwa uanze ndipo aende hospitalini.
Dkt Gembe kutoka
hospitali ya Meru jijini ARUSHA anasema tunawasaidia kinamama kuweza kugundua
dalili za mwanzo na tunawapa tiba na
tiba hii inapatikana mara baada ya mgonjwa kugundulika na dalili za mwanzo kama Mabaka meupe ambapo tunaanza na tiba
mgandisho.
Sr. Gladness John kutoka kitengo cha mahabara ya damu hospitali ya Mount Meru anasema, "hakika tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na wananchi wengi kumiminika na kutoa damu kutokana na kugusawa kwao na hali ya mama mjamzito kufariki kwa kukosa damu, hali hii inatia moyo sana na si kwa kinamama tu wanaojitokeza bali hata kinababa kama unavyoona nao wamekuja kwa wingi"





Post a Comment