DEVELOPIN STORY...
Serikali ya Afrika Kusini imechukua uamuzi wa
kuwafukuza raia wa kigeni waishio nchini humo kinyume cha sheria hatua hiyo
imepekea watu wakiofukuzwa nchini humo wakiwa ni kutoka nchi mbalimbali za
Afrika hususan raia kadhaa kutoka Nigeria.
![]() |
| PHOTO PROFILE: Mmoja wa raia aliyekamatwa na askali akipekuliwa kabla ya kupelekwa kunapohusika. |
AFRIKA KUSINI.
Vyombo vya habari nchini
Nigeria vimeripoti kuwa raia wapatao 97 wa nchi hiyo wanao tuhumiwa kuhusika na
uhalifu mbalimbali nchini Afrika kusini walifukuzwa toka siku ya Jumatatu.
Wizara ya mambo ya nje nchini Afrika Kusini
imethibitisha na kutoa ripoti kuwa raia kadha wa Nigeria wamefukuzwa kutoka
nchini humo huku raia wengine waliofukuzwa ni pamoja na wale kutoka Pakistan,
China, Bangladesh na Somalia.
![]() |
PHOTO
PROFILE: Baadhi ya raia wakiwa chini ya ulinzi.
|
Msemaji wa wizara hiyo Mayihlome Tshwete amesema kuwa,
mamia ya watu wasio na vibali walisafirishwa kutoka kurejea kwao na wengi wao ni
kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Afrika Kusini
inakumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka
yanayomilikiwa na wahamiaji.
Itakumbukwa kwamba serikali ya Afrika Kusini
huwafukuza kila mwaka watu wapatao 30,000 ambao wanaishi nchini humo kinyume
cha sheria au wale wanaohusika na mbalimbali nchini humo.


Post a Comment