![]() |
PICHA: Msaidizi wa mkaguzi mkuu wa Serikali Leonard Choti
Sendo akifungua warsha ya mafunzo kwa wakaguzi wa fedha wa ndani
(Internal Auditor) yanayofanyika jiji Arusha.
|
Picha By: Leonard Mutani.
ARUSHA.
Taasisi
isiyokuwa ya kiserikali JICA iliyojikita katika kusaidia nyanja mbalimbali za
maendeleo, kijamii, kiuchumi inaendesha mafunzo kwa wataalam wa usimamizi wa fedha
Wakaguzi wa serikali waliopo katika halmashauri nchini ili kuweza kuwa na uwezo
kwa kutumia njia za kisasa za kukagua ikiwa ni pamoja na muongozo wa vitabu vya
mafunzo (handbook sets) na kujua
mianya inayoweza kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.
Akifungua
mafunzo hayo ya siku nne na yaliyoshirikisha wakaguzi wa kanda ya kasikazini,
Msaidizi wa mkaguzi mkuu wa Serikali Leonard Choti Sendo amesema kuwa wakaguzi
kupata nafasi hii kukuza na kujenga uwezo wao yatawasaidia na kuwahakikishia
ubora wenye viwango kwenye utoaji wa huduma, ambapo kwenye mafunzo kama haya ndipo wanapopatikana wakaguzi wenye
weledi katika kusimamia fedha za halmashauri haliyopo.
“Baada
ya mafunzo haya, sasa wanaweza kupanga na kufanya kazi zao, kuweka kumbukumbu
zao vizuri na kuangalia mapungufu kwa weledi kuliko ilivyokuwa hapo awali,
mpaka sasa tupo wakaguzi mabingwa (Champions) 11, lakini kupitia mafunzo haya
tunatarajia tutaongezeka na kuwa wengi ili tuweze kuwa imara katika kusimamia
fedha za taasisi zetu” amesema Leonard.
Vilevile
Mkaguzi mkuu wa ukaguzi wa ndani na Mipango kutoka shirika la JICA nchin Shro
Otomo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuweza kujielekeza kwa umakini katika
matumizi ya dondoo za vitabu vinavyotoa muongozo hadidu (handbook sets) lakini kupitia vikundi vya
majadiliano hapo ndipo kila mtu ataweza kuuliza au kutoa uelewa kwa kile
anachokifaham.
Shirika
hili Japan International Cooperation Agency (JICA) lenye makao makuu yake nchini
Japan limekuwa likichangia kukuza ushirikiano na wa kimataifa na kutoa nafasi
ya kupaza sauti katika maendeleo kwa nchi nyingine ili ziweze kufikia uchumi
mkubwa ikiwa ni katika jamii na kuwa na ahueni au utulivu wa kiuchumi kwa kanda
zinazoendelea.
Post a Comment