Benki
ya Stanbic Tanzania imezikutanisha Taasisi na sekta mbalimbali za kirahia zisizo
za kibiashara na maendeleo katika jamii mkoani Arusha katika msingi wa uwezeshaji wa jamii kuweza kushiriki madhubuti kwenye
sekta zao za maendeleo na kuweza kuonyesha kujishugulisha kwa ustawi wa watu na maendeleo na uchumi wa Taifa.
![]() |
Msimamizi
wa washa ya taasisi na sekta binafsi akifungua washa kwa kusisitiza malengo ya
na majukumu ya kila muuzuliaji kuweza kujikita katika yale yanayozungumziwa.
|
![]() |
Washiriki
wa washa wakisikiliza mada ya awali inayoletwa na mleta mada kutoka taasisi ya
Angonet ya jijini Arusha.
|
![]() |
Abrie
Reutenbach Meneja wa kanda upande biashara za nje akitoa maelezo kuhusu
utendaji wa benki ya STANBIC kwa ukanda wa Afrika na jinsi ilivyojikita
kuwezesha taasisi na sekta ndogondogo.
|
![]() |
Katibu
mtendaji wa ANGONET Peter Bayo akielezea kuhusiana na majukumu
ya taasisi na asasi binafsi zinavyoweza kukuza uchumi kutokana na kuwa na
nafasi katika maendeleo ya nchi.
|
![]() |
Peter
Bayo kulia akimsikiliza Meneja wa Angonet na Meso Petro Ahhm alipokuwa
anachangia wakati wa mada iliyogusia wananchi kuweza kutumia nafasi yao kama
wazalishaji mali kuangalia na wakati.
|
![]() |
Kutoka kulia ni Abrie Reutenbach, Fredric Max, Steven Mpuya na Lawrence Mwandemani wakisikiliza mchango wa Petro Ahhm.
|
![]() |
| Steven Mpuya Afisa mkuu wa sekta za kijamii akieleza namna ofisi yake kupitia benki ya STANBIC ilivyojikita kuwezesha taasisi na sekta binafsi ili kufikia malengo ya uchumi. |
![]() |
Washiriki
wa washa wakisikiliza mada na kufuatilia maudhui yaliyotolewa na waleta mada kutoka kutoka STANBIC Benki jijini Arusha katika hotel ya Mount Meru.
|
![]() |
Mameneja wa matawi ya STANBIC wakiwa na meneja wa kanda ya Afrika katika Abrie Reutenbach.
|
Picha zote na TODAYS PRODUCTION
HABARI KWA UNDANI:
ARUSHA.
Katika
warsha hiyo mkurugenzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Angonet Peter Bayo
amesema kuwa pamoja na kuwepo nafasi kwa sekta binafsi kunyanyua uchumi kwa
njia ya jamii kujiwekeza moja kwa moja bado sekta hiyo imekuwa nyuma kutokana
na kutotambua nafasi yake kiujumla.
Vilevile aligusia uwezeshaji
wa asasi na wananchama kuweka mipango yao kama ndoto na maono yao ili
wanapoenda kutekeleza mipango yao wawe sawa, “maana asasi nyingi ni taasisi za kijamii
hivyo wanapenda baada ya muda na wao waweze kuona wamesogea mbele”.
Lakini wakati hali ya
taasisi na sekta binafsi zikiwa hazina uwezeshaji kutokana na kujikita zenyewe
pasipo kuangalia nafasi ya kuwatumia viongozi walio katika utashi kitaifa, bado
taasisi hizo zinatakiwa kuongea na mamlaka na watoa maamuzi, ikiwa na maana
kuna lasilimali ambazo bado hazijaonekana wakati zina mchango mkubwa katika
uchumi wa nchi.
Kwa upande wa uchumi
Afisa wa fedha wa benki ya STANBIC Zainul Chandoo amegusia kwenye uchumi wa nchi
na kusema kuwa taasisi za kiraia zina mchango kubwa japo Taasisi kubwa mbili za
Kilimo na Viwanda ndivyo zilizochangia kukuza uchumi mpaka sasa.
“kwa nafasi hatuwezi
kujitizama sisi wenyewe bali hata wengine wanaotuzunguka ikiwa ni pamoja
kuangalia maendeleo na uchumi ambao unategemea sana kile kinachozalishwa na
kuuzwa, kule kwenye mapato ya serikali (mapato ya ndani) tunategemea taasisi
zinazochangia kama taasisi za sekta binafsi ili kuweza kukuza uchumi” alisema Zainul Chandoo.












Post a Comment