0
Mafunzo ya siku tano yaliyokuwa yakitolewa na Taasisi ya RESCA ikishirikiana na serikali ya Marekani kitengo cha siasa na kupunguza ueneaji wa siraha nyepesi wametoa mafunzo yaliyohitimishwa leo kwa maafisa wa jeshi la polisi nchini kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania.

Mkufunzi mkuu Justin Pamba akiongea wakati wa kufungua hafla ya kufunga mafunzo ya siku tano kwa maofisa wa jeshi la polisi nchini yaliyofanyika jijini Arusha.

Meneja mipango wa RECSA Godfrey Bagonza kushoto, katikati ni Mratibu wa taifa wa SALW Charles Ulaya na kulia ni Dennis Hadrick Meneja mipango wa idara ya siasa na mambo ya kijeshi kutoka ofisi Marekani.

Meneja mipango wa RECSA Godfrey Bagonza pia aliweza kuongea wakati wa kufunga mafunzo hayo huku akiishukuru serikali ya Tanzania na Marekani kwa kuwezesha mafunzo hayo hapa nchini.


Dennis Hadrick Meneja mipango wa idara ya siasa na mambo ya kijeshi kutoka ofisi Marekani  akionyesha ramani ya Tanzania wakati wa kufunga mafunzo.

Baadhi wa maofisa wa jeshi la polisi waliokuwa katika mafunzo wakimsikiliza Capt Justin Pamba (mbele kushoto) alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi.
Mratibu wa taifa wa SALW Charles Ulaya katikati akimkabidhi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo sgt. Allen Daniel Mbwambo cheti cha maudhulio ya mafunzo hayo ya wiki moja, pembeni ni viongozi waandamizi.  


Dennis Hardrick kulia, Charles Ulaya, WP C. Gerald Minja wa pili kushoto akiwa na cheti cha maudhulio ya mafunzo mara baada ya kupokea cheti pamoja na Godfrey Bagonza.
Picha ya pamoja kwa viongozi, wakufunzi na wahitimu wa mafunzi ambao ni maofisa wa jeshi la polisi mara baada ya kukamilika kwa mafunzo na kukabidhiwa vyeti.





ARUSHA.
Katika mafunzo hayo yaliyokuwa yameegemea katika nyanja za utunzaji wa silaha kupitia maghala na zile zilizopo mitaani ambazo zimekuwa zikitumika kinyume na matumizi, yameendeshwa na wataalam wa mafunzo kutoka Kenya, Rwanda na Uganda ambapo kwa siku nne wamekuwa wakiwafunda kwa undani.

Justin Pamba ni  Mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo na mmoja kati ya waliofanikisha mafunzo hayo amesema “pamoja na kuwapa mafunzo hayo na kuwawezesha kufanikiwa kwa hatua nzuri na muda wote, vilevile malengo tuliyoweka kwa wahitmu hawa yamekwenda vizuri na kwa muda tuliopanga”


Dennis Hadrick Meneja mipango wa idara ya siasa na mambo ya kijeshi kutoka ofisi Marekani ametanabaisha jinsi mafunzo hayo yalivyofanyika kwa ustadi mkubwa wakati ambapo kuwakusanya maofisa wa jeshi kutoka mikoa yote nchini inaonyesha ukubwa wa Tanzania ambao inahitajika mafunzo hayo na wahitimu wakayafanyie kazi matokeo ya mafunzo hayo.


"yalikuwa mafunzo muhimu na yenye weledi wakati wote wa mafunzo ambapo lazima wahitimu muonyeshe kwa wale ambao hawakufika katika mafunzo kuwa nyie ni tofauti na wao, mnarudi katika viyuo vyeni vya kazi hivyo mkawe mabalozi na watendaji mtakaowezesha ujuzi mlioupata ukawe ni chachu ya utendaji wenye tija" alisema Dennis Hadrick.

Watoaji wa mafunzo hayo wametoa kila kitu kwa wahitimu wa mafunzo hayo ili kuhakikisha kuwa kile walichotoa kinaleta nafasi kwa wahitimu kuwa walimu kwa wenzao hususani kwa upande wa utunzaji wa maghala na silaha kwa ujumla.

Akifunga mafunzo hayo wakati wa utoaji wa vyeti kwa wahitimu wapatao 37 mgeni rasmi Mratibu wa taifa wa SALW Charles Ulaya amewashukuru wakufunzi kwa moyo wa dhati kufanikisha mafunzo na kwa ustadi mkubwa, "pamoja na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya marekani kwa kuunga mkono ambapo SALW imeweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi".



Post a Comment

 
Top