Bodi
ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB) inatarajiwa kufanya ziara ya
kitaaluma katika mikoa takribani kumi kwa lengo la kuzungumza na umma wa
wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wanaosomea fani ya ugavi na ununuzi kwa umma sambamba na
mafunzo yatakayofanyika siku ya tarehe 25 februari mwezi huu jijini Dar es salaam.
![]() |
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya
wataalam wa ugavi na ununuzi nchini Godfrey Mbanyi (kulia) akitoa maelezo kwa kina
kuhusu elimu ya maadili kwa wanahabari hawapo pichani.
|
![]() |
Kaimu mkurugenzi wa mafunzo Aman
Ngonyani akiongelea namna mafunzo yatakavyotolewa kwa mikoa kadhaa ili kuweza
kuwafikia wanaotarajiwa kufikiwa kwa muda usiopungua miezi miwili.
|
DAR ES SALAAM.
Akizungumza na wanahabari
leo jijini Dar es salaam kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalam wa ugavi
na ununuzi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi amesema ziara hiyo inalenga kuwaelimisha
wanafunzi wa fani hiyo juu ya maadili ya ugavi na ununuzi wa umma,
Vilevile katika mafunzo
hayo yatakayotolewa kwa viongozi wote pamoja na jumuiya za wanafunzi wa ununuzi
na ugavi yatawajengea uwezo wa kuwaandaa kulitumikia Taifa kwa uzalendo pindi
watakapomaliza.
Aidha bwana Mbanyi ameongeza
kuwa ufanyaji wa mitihani ya kitaaluma chini ya mtaala uliothibitishwa na
taasisi za kimataifa pamoja na majukumu ya bodi ya usajili kwa kuwajengea uwezo
wa kuwa na mawazo chanya ili kujenga uchumi wa viwanda nchini.
Wakati huo huo bodi
hiyo inatarajia kuendesha kongamano la siku moja la vijana ambao wanasomea fani ya ununuzi na ugavi
nchini, Sambamba na kongamano hilo, bodi hiyo inatarajia kutembelea vyuo vikuu
mbalimbali nchini vinavyofundisha masomo ya ugavi na kutoa mafunzo. Akivitaja
vyuo hivyo ni chuo cha usafirishaji (NIT) cha
Dar es salaam, CBE Dodoma na Mwanza, chuo kikuu cha
Jordani na Mzumbe vilivyopo mkoani Morogoro.
Vyuo vingine ni pamoja
na Uhasibu Mwanza, (TIA)Mbeya na Mtwara,
St.John na UDOM vilivyopo Dodoma, IAA
na Chuo kikuu cha Arusha, SMMUCO
na Mocu vya Moshi, Green Bird kilichopo Mwanga Kilimanjaro, RUCU
Iringa na SAUTI kilichopo Mwanza na
Mtwara.



Post a Comment