0
PHOTO PROFILE: Mmoja wa raia wa kigeni aliyepewa
adhabu kwa kuchomwa moto nchini Afrika kusini.
AFRIKA KUSINI:
Afrika Kusini inakabiliwa na kile tunachoweza kusema au kinachoelezwa kama vurugu  za kibaguzi, ambapo wenyeji wanadai wageni hao wamechukua ajira zao pamoja na kuwalaumu wakihusika kwa kiwango cha juu cha uhalifu.




PHOTO: Raia huyu wa Afrika kusini alikumbwa na
dhahama ya kipigo kabla ya kuonyesha kitambulisho. 

Watu wapatao milioni mbili ambao ni wageni wanaishi nchini Afrika Kusini na wengi wao walizaliwa katika nchi nyingine za Afrika, ikiwa ni pamoja Zimbabwe, Nigeria na Somalia, siku ya Ijumaa, polisi walitumia risasi za mpira na mabomu ya machozi kutawanya maandamano kwenye mji wa Pretoria wakati waandamanaji walipokuwa wakipambana na wahamiaji.


Hata hivyo Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma amelaani vurugu hizo na amesema mamlaka zinazohusika zinapaswa kufuatilia kujua wafanyakazi wasiokuwa na nyaraka muhimu zinazowataka kufanya kazi nchini humo. 

Post a Comment

 
Top