0
“Kweli nitakwenda Alhamisi, niko tayari kupimwa na kusachiwa. Lakini ningependa na Makonda apimwe pia na kusachiwa"

PHOTO: Profile Yusuph Manji.


Mfanyabiashara mashuhuri ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji leo anakwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha jijini Dar es Salaam kutokana na kutajwa katika majina ya wahusika katika skendo dawa za kulevya.

Taarifa hii ni baada ya jana kutoa taarifa kuwa atakwenda kituoni hapo leo badala ya kesho ambapo ni baada mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kutangaza majina 65 ya wanaitakiwa kufika kwenye kituo hicho cha Polisi ili kusaidia vita ya kupambana na madawa ya kulevya.

Katika taarifa yake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Manji alisema kuwa  hawezi kubadili ratiba zake keshokutwa na kwenda kupanga foleni ya watu 65 kwa ajili ya jambo hilo, alisema, ana kazi nyingi za kufanya siku hiyo ya ijumaa, hivyo ataenda leo mapema asubuhi ili kutekeleza wito.

Pamona na hilo Mfanyabiashra huyo ameongeza kwa kusema " napanga kuchukua hatua za kisheria kwa kwenda mahamakani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Makonda, mimi nitaenda kituo cha Polisi kesho (leo) asubuhi na mapema na sisubiri hiyo Ijumaa anayotaka yeye Makonda naomba nieleweke"

Mfanyabiashara huyo alisema kuwa hakatai kuwepo kwa vita ya kupambana na madawa ya kulevya, lakini huwezi kufanya kila kitu bila kujali haki za watu, hesbima, majina yao, "hali hii siwezi kukubali".

Post a Comment

 
Top