0
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye jana amesherehekea sherehe ya miaka 93 ya kuzaliwa kwake, ndiye kiongozi mkongwe kukaa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi duniani kwa mara ya kwanza hivi karibuni amezungumzia utawala wa Rais wa Marekani wa Donald Trump kwa kusema kuwa  anakubaliana na sera ya rais huyo kuwa "Marekani iwe ya Wamarekani", japo alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 93. 
ZIMBABWE.
Hata hivyo, amesema hakutaka pia "Madam Clinton ashinde", akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton, "Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo... Marekani iwe ya Wamarekani, katika hilo, nakubaliana naye na Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,"   Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald.
Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake, "Sijui ila mpeni muda bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe," amesema.

Grace Mugabe kulia akiteta jambo na Mumewe Robert Mugabe kushoto.
Hivi karibuni mke wa Rais huyo bi Grace Mugabe ambaye ana miaka 40 akiwa ni umri nusu kwa Mugabe, aliuambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura alisema watu wa Zimbabwe wanampenda Rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Bw Mugabe pia amesema anafaa kuendelea kuongoza, kwani watu wengi nchini mwake wanahisi kwamba hakuna mtu anayetosha kuchukua pahala pake, kiongozi huyo tayari ameteuliwa na chama tawala cha Zanu-PF kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ambapo ameiongoza Zimbabwe tangu uhuru mwaka 1980.

Post a Comment

 
Top