Developing Story.
“Tusishabikie shabikie
kwa wepesi suala hili la dawa za kulevya, nimekuwa nikiangalia maneno kwenye mitandao,
mengine yanasikitisha sana, hii vita kama zilivyo vita zingine tusichukulie
kimzaha, madhara yake ni makubwa”
![]() |
PROFILE PHOTO: Rais John Pombe Magufuri. |
“Mtu anakwenda polisi kulipoti alafu wengine wanapiga deki gari, kwani mliambiwa hapo ni kwa kusafisha magari?, na polisi mpo hapo tu, shika wote ikiwezekana na gari weka lock up. Mtu anapeleka kwaya mliambiwa mnakwenda kuimbiwa mapambio, I wish I could be IGP, sasa sitaki kitokee kitu cha namna hiyo. Mambo ya msingi tunaweka mzaha, mbona hamkwenda lugaro kuimba? Tunataka vyombo vya ulinzi viheshimiwe, tukileta mzaha tutakuja kujuta huko mbele.”
“Wale wote
waliohukumiwa nje ya nchi ya nchi, wawe wakehukumiwa kunyongwa au kufungwa
maisha, Waziri wa mambo ya nje na mabalozi wetu msijihusishe katika kitu
chochote. Waachani wapate wanachostahili. Kama amefungwa kwa dawa za kulevya na
akahukumIwa kunyongwa mwache anyongwe”
“Pamoja na kwamba
sheria ilipitishwa, Waziri mkuu hakujua kama yeye ni mwenyekiti, alifichwa.
Waziri mkuu kama amejua basi amejua jana au juzi kwamba yeye ni mwenyekiti wa
balaza linalohusika katika kuzuia na kupambana na dawa za kulevya”
“Hata mimi sikuletewa
mapendekezo ya kumteua Kamishna mkuu mpaka nikaamua kumteua. Ni lazima tuzungumze
ukweli, kwa ni tukificha tutajifanya malaika, sijaletewa niliamua kuteua
mwenyewe. Kwa hiyo mnaweza kujua kwa namna ganivita hii ilivyokuwa kubwa”
“Sheria namba 5 ya mwaka 2015, tumepewa
mamlaka sisi serikali ya kupambana na dawa za kulevya, hatutojali mtu yeyote,
awe mbunge, waziri, mwanasiasa. Polisi, mwanajeshi, mtoto, mkubwa, mchingaji,
padre, au sheikh tutadeal naye na hili nataka kusema kwa dhati”
“Nawapongeza wabunge
waliopita chini ya Spika mama Anna Makinda, walikaa bila kujali vyama vyao na
kupitisha sheria namba 5 ya mwaka 2015 ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya. Vilevile
nampongeza Rais mstaafu Jkaya Kikwete kwa kupata uchungu kwa watanzania
waliokuwa wakiumia kwa kuweka saini ya matumizi ya sheria hii Mei 11,2015 hivyo
sisi tunawajibu wa kusimamia, hatutorudi nyuma”
“Majeshi ya ulinzi na
usalama, Jeshi la wananchi, Polisi, Uhamiaji, TISS, Magereza na Zimamoto, wote
mkasimamie kazi hii"
Post a Comment