Changamoto za maisha, ugumu wa maisha, njaa, hali
mbaya ya hewa, mfumo wa maisha, kukosekana kwa ajira na mengine yanayotokea
katika baadhi ya nchi yanapelekea baadhi ya raia wa nchi husika kuona hakuna
unafuu wa kuendelea kuishi hapo alipozaliwa na hii inatokea mpaka sasa.
![]() |
Huyu alifichwa kwenye eneo la mbele la gari /dashboard/ ili avuke
mpaka kwenda kutafuta maisha. |
![]() |
Hii ni picha ambayo maofisa walipiga kuonyesha uharisia wa kile
kinachotokea
kwa wahamiaji hao, jamaa alifungiwa kwenye sanduku. |
![]() |
Unaweza kupiga picha kupata taswira ni jinsi gani mtu anaweza kukunjwa
na kuwekwa kwenye kiti ili kujificha kwa lengo flani. |
Wakati
maofisa hao walipokuwa wanakagua gari moja siku ya Jumatatu, walimkuta mtu
mmoja amefichwa kwenye eneo la mbele la gari (dashboard) na mwengine amefichwa
kwenye eneo la kiti cha nyuma cha gari.
Mwanamme
na mwanamke wanaodaiwa kuwa raia wa Guinea walipewa huduma ya kwanza kwa kuwa
walikuwa na hewa kidogo ya kupumua iliyowafanya kuchoka na kudhoofu. Katika tukio lingine kwa raia kuendelea
kutafuta maisha kwa kwenda nchi nyingine kwa njia za hatari kijana mmoja mwenye
asili ya kiafrika alipatikana amefichwa kwenye sanduku la mwanamke.
Kisa
hicho kilitokea mnamo mwezi disemba 30 na mtu huyo anayeaminika kutoka Gabon
alihitaji matibabu ya dharura. Vile vile mwanamke mwenye umri wa miaka 22
kutoka nchini Morocco yeye alijaribu kumuingiza Cueta, lakini maofisa wa
uhamiaji walimuagiza kufungua sanduku lake ambalo lilikuwa limefungwa kwenye
kitoroli.
Kisa hicho kinajili wakati ambapo
kumekuwa na majaribio ya wahamiaji wengi kuvunja ugo wa mita sita unaogawanya
Cueta na Morocco, raia wapatao 50 wa Morocco na 5 wa Uhispania walijeruhiwa
wakati wahamiaji 1,100 walipojaribu kupita wigo huo na kuingia Cueta kutoka
Morocco.
Source BBC
Post a Comment