Developing Story;
Wakati idadi ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya nchini ikiendelea kuongezeka huku vijana wengi na hata ukanda wa Afrika mashariki wakiona ndiyo suluhu ya kumaliza matatizo yao, Serikali imeanzisha msako dhidi ya wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya nchini humo.
Wakati idadi ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya nchini ikiendelea kuongezeka huku vijana wengi na hata ukanda wa Afrika mashariki wakiona ndiyo suluhu ya kumaliza matatizo yao, Serikali imeanzisha msako dhidi ya wauzaji na waingizaji wa dawa za kulevya nchini humo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na msanii wa Rehema
chalamila
Ikulu wakati alipopata msaada kuondokana na matumizi ya dawa
hizo.
|
Kuathirika kwa
mwili kutokana na kuendelea kutumia dawa za kulevya uhathili mwili, kara nyingi
sindano za mara kwa mara zinaweza kusababisha mishipa kusinyaa na uweza
kusababisha maambukizi ya mishipa ya damu na valves za moyo. Haya ni baadhi ya
matokeo ya muda mrefu ya matumizi ya madawa ya kulevya aina ya heroin.
Watumiaji wa madawa
aina ya heroin mara nyingi uchangia sindano ambapo hali hiyo inapelekea
kuongozeka kwa ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza.
Hizi ni sura tofauti za
watu waliothirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, jamii inapata
wakati mgumu kuwasaidia watu wa aina hii wakiwa wameathirika kutokana na
matumizi.
Hapa nakupa kwa
udondozi/kidogo kuhusu madhara yanayomkuta mtumiaji;
Meno
kupoteza uharisia kuwa mabaya, kuvimba fizi, kuwashwa, kudhoofika kwa mfumo wa
kinga, udhaifu wa misuli/kupooza, kupungua uwezo wa kijinsia na wa muda mrefu
Impotence kwa wanaume, matatizo ya hedhi kwa wanawake, uwezo wa kufika/orgasm
pande zote (wanawake na wanaume), kupoteza kumbukumbu na utendaji wa akili, kupoteza
hamu ya kula.
UPDATES from 04.01.2017: Baadhi ya wazazi waliozungumza wamesema kuwa, mbali na kuwa na jukumu kubwa la kudhibiti vijana kujitumbukiza kwenye matumizi ya dawa linaanzia katika ngazi ya familia, wanasema Serikali pia inao mchango mkubwa katika kuwakabili waingizaji na wauzaji wa dawa hizi.
Kamishna wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya nchini
ACP Mihayo Msikhela, amesema kuwa kitengo chake kimeanzisha msako maalumu dhidi
ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya pamoja na wale wauzaji wadogo, ili
kuhakikisha wanazuia mianya yote inayotumiwa na wauzaji hao kuzifikiza dawa
hizo nchini.
Kamishina Msikhela, amekiri kuwa janga la dawa za
kulevya nchini Tanzania ni kubwa na juhudi za makusudi zinaendelea kufanywa na
Serikali katika kuhakikisha wahusika wa biashara hii haramu wanakamatwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Profile Photo: Waziri wa mambo ya ndani ya nchi; Mwigulu Nchemba. |
Kwa upande wake waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mwigulu Nchemba, amesema hali hiyo haikubaliki na kwamba wao kama wizara tayari
wameanza mikakati madhubuti kuhakikisha wanawanusuru vijana hawa dhidi ya
matumizi ya unga, ikiwa ni pamoja na kuwasaka wauzaji wenyewe.
Kwa upande wao viongozi wa dini mbali na kuitaka jamii
kubadili mtazamo kuhusu familia, wanasema ni jukumu la kila mtu kuhakikisha
wanawasaidia vijana kiimani ili kuwaondolea dhana kuwa unga ndio suluhu ya
matatizo na badala yake watafutiwe vitu vingine vya kufanya ambavyo
vitawaepusha na utumiaji wa dawa.
Kwa mujibu wa tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini,
kiwango cha dawa zinazoingia na kukamatwa kimepanda kutoka kilo tatu za dawa
aina ya Heroin mwaka 2008 hadi kilo 265.54 mwaka 2011 na kile nne za dawa aina
ya Cocaine hadi kufikia kilo 128.30 mwaka huo huo.
Post a Comment