Inakumbukwa
Aprili 15.1912 ambapo meashua kubwa ya Titanic ilishuka ndani ya bahari
ya Atlantiki kaskazini ikiwa ni 400 maili kusini mwa New foundland, Canada
mashua ambayo iliweza kubeba abiria 2,200 wakiwamo wafanyakazi. Mashua hiyo ilikuwa katika safari
yake ya kwanza ikitokea Southampton kuelekea NewYork nchini Marakani.
Historia inaeleza mambo
mengi ikiwamo baadhi ya mashirika makubwa, wafanyabiashara na makampuni ambayo
yaliwahi kujitokeza kutaka kuunda mashua sawia kama ile Titanic, lakini
hawakuweza kufikia malengo kutokana na sababu ambazo hazipo wazi.
Baada ya kusaini mkataba maalum wa kuanza ujenzi.
|
Ujenzi wa awali ukianza kwa wataalam kupanga sakafu.
|
Bilionea mmoja kutoka
Australia, Clive Palmer, alitangaza mipango yake ya kutengeneza mashua kama ya
Titanic mwaka 2012, lakini mradi huo mpaka leo bado haujakamilika.
Mashua ya Titanic
iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast, iligonga mwamba wa barafu na
kuzama kaskazini mwa bahari ya Atlantic mnamo mwaka 1912 hatua iliyosababisha
vifo vya zaidi ya watu 1,500.
Nchini china ujenzi wa mashua sawia
na Titanic umeanza siku ya Alhamisi iliyopita ujenzi huo wa mashua hiyo yenye urefu wa kina cha mita
269, itawekwa katika hifadhi iliyoko maeneo ya kijijini/mashambani katika mkoa
wa Sichuan. Baada ya taarifa za ujenzi wa mashua/meli hiyo kusambaa
iliwashangaza raia wengi China.
Eneo inapojengwa mashua hiyo lililo mkoa wa Sichuan China |
Kampuni iliyobuni
mradi huo mkubwa Qixing Energy Investment Group ilitangaza mipango wa mradi huyo,
utakaogharimu Yuan bilioni moja mwaka 2014, kulingana na shirika la habari la CNA.
Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic,
itakuwa na uwanja wa michezo, sehemmu ya kuogelea, maonyesho, maduka, mitaa ya
watu maalum na itakuwa na mtandao wa Wifi huku ikitarajiwa kuwa kivutio kikubwa
katika eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Msomaji wetu ukiwa na tatizo la kutokuona picha kwa muonekano halisi kupitia kifaa chako tafadhali tuandikie maoni yako: 0773036064
Post a Comment