0
Rais wa Cuba Raul Castro
kulia akitoa 
 salamu za mwisho.
Wakati wananchi wa Cuba wakiwa na majozi ya kuondokewa na kiongozi wao marehemu Fidel Castro, baadaye mapema leo mwili wake ukiwa umechomwa moto na kuwa jivu  limezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, hivyo kumaliza takribani siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.

Familia na baadhi ya wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa nchi ya Cuba, Jose Marti.

Wakati wa kuaga mwili kwa siku ya jana, Rais wa sasa wa Cuba ambaye ni mdogo wake Fidel Castro, Raul Castro, amesema serikali yake haitatoa au kuweka kumbukumbu ya barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Marehemu mwenyewe alivyoagiza kabla hajafariki.

Mbele ya umati mkubwa wa watu kwenye mji wa Santiago, alisema Fidel Castro hakupenda kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.


Wananchi wa Cuba wakitoa salamu za mwisho kwa kuuaga mwili wa marehemu Fidel Castro mapema leo.

Mwili wa marehemu Fidel Castro mara baada ya kuagwa na wananchi, viongozi mbalimbali unapelekwa katika mji wa Santiago kwa ajili ya maziko ramsi.



Post a Comment

 
Top