Afisa
mipango anayeshugulikia kanda Rutendo Tinanuo akielezea namna kanda yake
inavyoweka jitihada kwa kuhamasisha washirika wake kuzalisha na kuweka mkazo
katika upande huo.
|
HABARI ZAIDI:
Leonard Mutani -Arusha
Mkutano wa kikanda wa siku mbili unaohusu chakula na
kilimo wa shirika la umoja wa mataifa UN (FAO) unafanyika jijini Arusha ukiwa
na dhumuni la kuboresha usalama wa vyakula unazalishwa, kuuzawa na unaoingizwa kwenye
nchi jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na nchi wanachama wa COMESA pamoja na
zile za IGAD.
Akiongea na TODAYS NEWS mshauri mstaafu na
mwenyekiti wa Codex Dr. Claude John Shara anasema “usalama
wa chakula unapaswa kuangaliwa tokea ununuzi wa mbegu, upandaji, uvunaji,
usafirishaji mpaka kwa mlaji ili kuweza kuwa na chakula chenye usalama”.
Mkutano huo ulioshirikisha zaidi ya mataifa ishirini
na tano na mashirika na taasisi binafsi, pia kwa hapa nchini umeshirikisha
wataalam wa sekta mbalimbali, mmoja wapo ni Afisa wa kilimo na chakula kutoka
Wakala wa vipimo nchini (TBS) Lazaro H. Msasalaga ambaye anasema,” kwa mujibu wa sheria ya viwango ya mwaka 2009 shirika
la viwango (TBS) lina majukumu ikiwemo
kuandaa viwango vya kitaifa vinavyoweza kutumika na taasisi mbalimbali, ili
kuahakikisha usalama wa chakula unakuwepo nchini”
Pamoja na kuwepo taasisi shirika hilo bado
kumekuwepo na kamati mbalimbali zinazofikia 30 zinazowiana na kamati za
kimataifa mfano Codex international na nyingine ambazo pia ushirikisha wadau
wengine vikiwemo vyuo vikuu, mashirika binafsi na wengine ambao ni wataalam
wababezi katika masuala ya chakula na kilimo.
Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) pamoja na
kuwa shirika mama duniani linaloratibu na kuangalia upatikanaji wa chakula duniani
bado limekuwa mstari wa mbele kuratibu upatika ji wa chakula chenye usalama kwa
viwango vya kimataifa, Willy Musinguzi Afisa wa viwango wa kanda (EAC) anasema
wao wana majukumu ya kuweka mazingira yanayoweza kutekeleza kufanya biashara
katika ukanda awa kitaifa na kimataifa , “kama
wasambazaji wetu hawatafuata viwango vinavytakiwa basi vyakula vyao
vitakataliwa.”
Pamoja na kuunganisha mashirika mbalimbali
uborshwaji na upatikanaji wa vyakula katika nchi za ukanda wa afrika mashariki
unahitaji mfumo wa uthibiti mzuri pamoja na kukumbwa na magonjwa kama sumu kuvu
kwa baadhi ya mimea lakini pia hmabadiriko ya tabia nchi yanayopelekea
kutopatikana kwa mvua za kutosha ili kuweza kupata cha kutoshwa kwa wananchi wa
ukanda huu wa Afrika ya mashariki.
Post a Comment