Serengeti Natinal Park Photo by Leonard Mutani |
Elimu ni kituo cha kumpa mtu ufahamu kuhusiana
na jambo flani ambalo uenda analifaham au halijui, kupitia TODAYS NEWS mara
kadhaa tutakuwa tukikuletea mambo kadha wa kadha kuhusu maliasili zetu ikiwa ni
siku chache tu zimepita chama kijulikanacho kama JOURNALIST FRIEND OF WILDLIFE AND HERITAGE kimezaliwa na kupewa hati ya kutambulika.
Waandishi kadhaa,
pamoja na wadau mbalimbali wa Tasnia ya Mazingira, Uhifadhi, Wanyamapoli na
mambo yahusuyo Urithi wa dunia tutakuwa bega kwa bega kukupa habari kiundani.
Nini maana ya Uhifadhi ?
Kutunza,
kulinda na kusimamia maeneo maalum yaliyotengwa kisheria kwa ajili ya
wanyamapori na maliasili nyingine kama misitu, maji, madini na viumbe waishio
majini hiyo ni sehemu ya Uhifadhi.
Historia
ya Uhifadhi Tanzania inaanzia mwaka 1891 mpaka 1961pale ambapo Tanzania Bara
ilipopata uhuru na wakati huo wote nchi ilitumia Sheria za kikoloni katika masuala
ya uhifadhi.
Mnamo
mwaka 1961lilitolewa Azimio la Arusha na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
ambaye ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kupitia Azimio hili
alisema…
“Uhai wa Wanyamapori ni jambo linalotuhusu sote katika Afrika.
Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi, sio muhimu tu kwa ajili
ya kustajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali
wa maisha yetu ya baadaye.
Kwa kukubali dhamana ya wanyamapori wetu tunatamka kwa dhati kwamba
tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba wajukuu wa watoto wetu wataweza kufurahia
urithi huu mkubwa na wa thamani adimu.
Uhifadhi wa wanyamapori na maeneo yote yenye mapori huhitaji maarifa
ya kitaalamu, wafanyakazi waliopata mafunzo maalumu, na fedha, hivyo tunaomba mataifa
mengine yashirikiane na serikali katika kazi hii muhimu, ambayo kufanikiwa au
kutofanikiwa kwake hakuathiri tu Bara la Afrika bali ulimwengu mzima kwa ujumla.”
Hata
hivyo, kuanzia mwaka 1961 hadi 1974 Azimio la Arusha la Uhifadhi lilitumika kama
Mwongozo katika shughuli zote za uhifadhi. Kama ambavyo utaona katika Azimio hili
kwamba;
· Limezungumzia Ushirikishwaji katika
uhifadhi.
· Utalii na urithi wa
rasilimali na makazi yao.
· Limetoa hamasa ya kutoa mafunzo au kutambua umuhimu wa mafunzo na utaalam.
· Limetia mkazo wa usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori kwa
ajili vizazi vya sasa na vijavyo.
· Linasisitiza matumizi endelevu ya
rasilimali ya Wanyamapori.
· Azimio hilo pia limetoa wito kwa mataifa
mengine kutuunga mkono.
Azimio
hili limetumika kwa muda mrefu, hata hivyo kutokana na changamoto za mabadiliko
ya kiuchumi, kiteknolojia na kijamii ilionekana kuwa kuna umuhimu wa kutunga
sheria na baadaye ndipo Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na 12 ya mwaka 1974 ilipotungwa.
Sheria
hii ilifanyiwa marekebisho au mapitio na kuzaa Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori
Na 5 ya mwaka 2009 pia sera ya wanyamapori ya 2007. Sheria hizi zote pamoja na
sera zilikuwa zinahakikisha na zinazingatia tamko la Azimio la Arusha.
Imeandaliwa na Leonard Mutani kwa msaada wa Twaha Twahibu wa wizara ya maliasili na Utalii.
Post a Comment