Rais wa JMT Dr. John Pombe Magufuri. |
Hatimaye Rais John P.Magufuri amesaini muswada wa habari huku akitanabaisha kuwa utakuwa na manufaa kwa wanahabari pamoja na kuwa na tija kwa sekta ya habari kwa mustakabali wa taifa.
Taarifa iliyotolewa jana na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ilisema, Rais alisaini muswada wa sheria ya habari ya mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 katika mkutano wake wa 5 uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
Katika kauli yake alipokuwa akizungumza na wahariri na wanahabari ikulu jijini Dar Es Salaam, Rais Magufuri aliweka wazi kuhusaini mara moja mara muswada huo utakapopelekwa kwake. Hata hivyo amewashukuru wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa muswada huo.
Post a Comment