Watoto kuzaliwa kuwa si wakawaida na vichwa vyenye muonekano tofauti. |
Japokuwa maafisa wa
afya ya jamii na watafiti wamefanikiwa katika kuelewa na kudhibiti virusi vya
Zika, shirika la Afya duniani (WHO) linasema virusi hivyo vitaendelea kuwepo
kwa muda mrefu na lazima ushughulikiwe likiwa kama tatizo la muda mrefu.
Mambo kadha machache
yalijulikana kuhusu ugonjwa huo wakati shirika la Afya duniani WHO lilipotangaza
virusi hivyo kuwa ni tatizo la dharura kimataifa kwa afya ya jamii ya mnamo
mwezi Februari mwaka huu.
Toka wakati huo, idara
ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia majanga ya dharula limejifunza kwamba,
virusi hivyo vitaendelea kusambaa na kusababisha tatizo lijulikanalo kitaalam “microcephaly” linalosababisha
ubongo kutokuwa wa kawaida kwa watoto wachanga.
Aina ya mbu anayeharibu ubongo wa mtoto na kusababisha madhara. |
Kwa upande mwingine
mkurugenzi mtendaji wa WHO anayeshugulikia mambo ya dharura za afya, Peter
Salama, anasema suala kubwa kuhusu virusi hivyo bado halijulikani, na
linahitaji kufanyiwa utafiti kwa undani zaidi, akaongeza mipango ya sasa ya
dharura itabadilishwa kuwa ya kati na muda mrefu kwa kazi ambayo itazungumzia
masuala mengi ambayo hayajashughulikiwa.
Anthony Costello ni
mkurugenzi wa Afya ya uzazi, watoto wachanga, na Afya ya watoto, anasema Zika
haitoweza kuwa dharura tena katika afya ya jamii kutokana na namna
inavyofahamika miongoni mwa watu, lakini bado ni tatizo kwa baadhi ya nchi huku
kukiwa na wasiwasi mkubwa duniani.
Shirika la afya duniani
(WHO) linahitaji dola milioni 112 kutekeleza mipango ya kuzuia hama kutokomeza
virusi hivyo mpaka mwakani, ikiwa mpaka sasa, imeshapokea dola milioni 50,
ikikaribia nusu ya bajeti inayohitajika katika mpango huo.
Hata hviyo linasema linajipanga
kufanya kazi kusaidia nchi zinazopambana na virusi vya zika huku likisaidia
kuandaa mifumo ya uangalizi ili iweze kufuatilia na kutambua virusi na
kuvifuatilia kwa ukaribu, pia litafanya kazi na nchi zenye zilizoathilika ili
kuboresha na kuimarisha mipango yao ya majibu ya kitaifa ya kupambana na virusi
hivyo.
Post a Comment